'Ngojeni basi nipewe talaka,'Nyota Ndogo agadhabishwa na wanawake wanaomtumia mumewe jumbe

Muhtasari
  • Nyota Ndogo awaonya wanawake wanaomtumia mumewe jumbe

Msanii Nyota Ndogo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewakashifu na kuwaonya wanawake ambao wamekuwa wakimtumia mumewe jumbe.

Hii ni baada ya wawili hao kuachana kutokana na utani wake msanii huyo siku ya 'Fools day'.

Siku chache zilizopita msanii huyo alimsihi na kumuomba mumewe amrudie kwani alikuwa tayari amejifunza kwamba hawezi ishi bila mapenzi yake.

 

Kupitia kwa video aliopakia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alionekana kugadhabishwa na tabia ya wanawake hao.

Bali na kugadhabishwa na tabia za wanawake hao aliwashauri waweze kujaribu bahati yao kama wanamktaka mumewe lakini wangoje apewe talaka.

"Sasa wa mama mumebakia na kunijadili mavazi na viatu. Kila mtu avae apendavyo kisha mimi mtu mzima swali ni natoshana na mamaako?nyooooo kumbe furaha yetu kuona watu wakiteseka yani muko bizi very bizi kunitukana

Wake za watu na galfriends za watu wamejaa inbox ya mume wangu basi si musubiri hata nipewe talaka wengine hata wamenivamia sura yangu nyinyi wenye sura nzuri munajiona munaenda HEVENI?

..afadhali sura mbaya mwenye akili kuliko urembo akili amekalia wala sijuti haya ukumbi wenu endeleeni ila inbox kwachekesha watu wanajichetua Jamani

LAKINI MUSIJALI SIWEZI KUTAKA KUVUNJA NDOA YA MTU SO SIWEKA WAZI AKIKISHENI USINGIZI MUNAPATA," Aliandika Nyota.