'Si kuzaa kawaida nilifanyiwa upasuaji,'Lilian Muli afichua

Muhtasari
  • Lilian Muli afichua alijifungua kwa njia ya upasuaji
  • Muli alisema alijifunza mengi kutokana na mahusiano yake ya kimapenzi ambayo aliyapitia awali na kwa sasa hana mpango wa kuwa na mpenzi tena
Lillian-Muli-new-look-696x418
Lillian-Muli-new-look-696x418

Mwanahabari wa runinga ya Citizen LIlian Muli kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram katika sekta ya maswali na majibu alifichua mambo kadha wa kadha katika maisha yake.

Muli alisema alijifunza mengi kutokana na mahusiano yake ya kimapenzi ambayo aliyapitia awali na kwa sasa hana mpango wa kuwa na mpenzi tena.

Mmoja wa mashabiki wake alimuuliza kuhusu mapenzi, biashara na watoto na hili ndilo lilikuwa jibu lake

" Haya ni maswali ya kibinafsi na ya faragha, niliamua maisha yangu yawe hivyo."

Aidha, Muli alisema huwa hawaposti watoto wake kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu wangali wachanga na wakati utafika ambapo atafanya hivyo.

Mwanahabari huyo amebarikiwa na watoto wawili huku akifichua kwamba hajapanga kuongeza mwingine.

Alifichua hayo baada ya mmoja wa mashabiki wake kumuuliza kama ana mpango wa kuongeza mtoto mwingine.

Pia LIlian alifichua kwamba alijifungua kwa njia ya upasuaji na wala hakujifungua kwa nia ya kawaida.

Mwanahabari huyo alisema kwamba hana mchumba kwa sasa ana furaha na maisha yake jinsi alivyo.

"Nilikuwa nimeolewa lakini safari haikuwa njema, naonelea kwa sasa nafurahi maisha, nina furaha sana," Alisema Muli.