Tunajua vizuri sio dhoruba zote zinazokuja kutuangamiza-Mike Sonko

Muhtasari
  • KUlingana na mwanasiasa huyo sio wimbi au dhoruba zote zinazokuja  kuangamiza maisha ya mwanadamu bali huja kusafisha njia zao
  • Mwaka jana, na mapema mwaka huu Sonko alipitia changamoto  na kukabiliwa na mashataka tofauti huku akibaduliwa kuwa gavana wa kaunti ya Nairobi
  • Pia alimshukuru Mungu kwa yote ambayo amempigania na kumuonekania
Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko

Gavana wa zamani wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko amewasuta wale wote waliona ataangamiaKwa changamoto alizokuwa amepitia na kukumbana nazo.

KUlingana na mwanasiasa huyo sio wimbi au dhoruba zote zinazokuja  kuangamiza maisha ya mwanadamu bali huja kusafisha njia zao.

Mwaka jana, na mapema mwaka huu Sonko alipitia changamoto  na kukabiliwa na mashataka tofauti huku akibaduliwa kuwa gavana wa kaunti ya Nairobi.

Pia alimshukuru Mungu kwa yote ambayo amempigania na kumuonekania.

Watu wangu Asubuhi Njema,kwa maana Tunamtumikia Mungu mwaminifu anayesikiliza na kujibu maombi hatutachoka kumuomba

Mpendwa Bwana, Siwezi kukushukuru vya kutosha kwa kuniweka mimi na wafuasi wangu wote ninaowapenda kwenye ukurasa huu salama katika nyakati hizi ngumu

Ninaomba kwamba Uendelee kutubariki na kutulinda daima. Tunajua vizuri sio dhoruba zote zinazokuja kutuangamiza, wengine huja kusafisha njia yetu siku hizi watu wengine wanatuudhi kwa sababu hatuteseka kama vile walivyotutarajia. Bwana Naomba uendelee kuwakatisha tamaa. Tuko mikononi mwako.