Mchekeshaji Professor Hamo awaomba wanawe, mashabiki na familia msamaha

Muhtasari
  • Wiki chache zilizopita mchekeshaji wa kipindi cha churchill Professor Hamo na mcheshi Jemutai walivuma sana kwenye mitandao ya kijamii
  • Hii ni baada ya Jemutai kufichua kwamba Hamo hajukumikii wanawe ambao walibarikiwa naye
  • Mengi yalisemwa, huku asilimia kubwa ya mashabiki wakimkejeli mchekeshaji huyo kwa kuwacha wanawe wateseke
images
images

Wiki chache zilizopita mchekeshaji wa kipindi cha churchill Professor Hamo na mcheshi Jemutai walivuma sana kwenye mitandao ya kijamii.

Hii ni baada ya Jemutai kufichua kwamba Hamo hajukumikii wanawe ambao walibarikiwa naye.

Mengi yalisemwa, huku asilimia kubwa ya mashabiki wakimkejeli mchekeshaji huyo kwa kuwacha wanawe wateseke.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram mchekeshaji huyo aliomba wanawe,mashabiki na familia yake msamaha kwa yale walishuudia.

"Maisha yana njia ya kuingiza nguvu kwa mtu ndani ya hekima. Mengi yalitokea, mengi yalisemwa, chanya na hasi katika pumzi ile ile

Ikiwa kuomba msamaha kutafanywa basi inapaswa kutafutwa na roho, kweli, na kutoka chini kabisa

Msamaha hufanywa wakati mtu anatambua na anamiliki makosa yao. Ilinibidi nirudi kwa familia na kufanya vizuri nao vinginevyo hii yote ingekuwa sura ya mbele

Tunaunganisha vitu, sio huko bado lakini tumeelekea huko kwa neema yake," Aliandika Hamo.

Pia alimshukuru Jemutai kwa kukubaliana naye jinsi ya kuwalea watoto wao;

"Ningependa kumshukuru bosi wangu aliyekua mshauri, Bwana Daniel Ndambuki 'Churchill', na Kocha wa Maisha Robert Burale kwa kutujengea maarifa na hekima muhimu ndani yetu tukikunywa kale ka chai kamejaa maziwa miiingi ..!

Asante kubwa kwa Jemutai kwa kukubali sisi kukaa chini na kuwa na mazungumzo ya amani juu ya jinsi tutakavyowalea watoto wetu.

Asante maalum kwa Zippy bado ulinishughulikia licha ya ujio wangu mfupi. Kwa vijana wangu, maisha sio njia rahisi, baba anajuta sana na anatumai siku moja ukiwa na umri wa kutosha kuelewa utamsamehe."

Hamo alikiri kuwapenda wanawe, huku akiomba msamaha kwa mashabiki na kusema kwamba anatia bidii katika kazi yake ili awe mtu ambaye anawajibika majukumu yake.

"Nawapenda wotena nitahakikisha nipo hapa kwa ajili yenu 🥰. Familia ya RMS poleni kwa kuburuzwa katika haya yote unajua walikuwa hapa wiki 3 mapema

Na kwenu mashabiki wangu. Bila wewe mimi ni Herman tu. Pamoja na wewe mimi ni Prof Hamo

Niruhusu niongeze sura nyingine katika "Kitabu Changu Cha .." Samahani sana kwa kukuangusha

Bado sipo lakini ninafanya kazi kwa kuwa mtu anayewajibika, baba, mume na mtu. Mungu ni Mwema .. !!!,"