Niliogopa!Msanii Mercy Masika aeleza kwanini hakutaka ujauzito baada ya kuolewa

Muhtasari
  • Ni matamanio ya kila mwanamke baada ya kuingia kwenye ndoa kubarikiwa na mtoto, na kuitwa mama.
  • Kulingana na msanii wa nyimbo za injili Mercy Masika hakutaka kujifungua baada ya kuolewa kwa maana aliamini kwamba kujifungua ni uchungu
  • Ni jambo ambalo Mercy aliona ni uchungu huku akikiri kwamba alikuwa anaogopa sana
82165159_619911565463731_8777097389591686827_n(1)
82165159_619911565463731_8777097389591686827_n(1)

Ni matamanio ya kila mwanamke baada ya kuingia kwenye ndoa kubarikiwa na mtoto, na kuitwa mama.

Lakini kuna wale huwa na hofu katika maisha yao ya kujifungua, kwa mana wameamini kwamba ni jambo la uchungu kama vile wanavyoelezewa na wenzao.

Kulingana na msanii wa nyimbo za injili Mercy Masika hakutaka kujifungua baada ya kuolewa kwa maana aliamini kwamba kujifungua ni uchungu kama vile alikuwa ameambiwa na shangazi yake.

Ni jambo ambalo Mercy aliona ni uchungu huku akikiri kwamba alikuwa anaogopa sana.

Akiwa kwenye mahojiano alikuwa na haya ya kusimulia;

"Wakati wa mimba yangu ya kwanza nilidungwa sindano kwa maana nilikuwa katika uchungu usiku kucha

Nilikuwa naogopa sana kwa maana nilitarajia uchungu kama ule huwa naona wanawake wakiwa nao katika filamu lakini hayo hayakutendeka

Hiyo ndio maana sikutaka watoto kwa maana kwa akili yangu ilikuwa uuuiii watakurarua, kama mtoto unaona kujifungua ni drama lakini sikujua nilijifungua aje

Nilikuwa tu natabika, na kuahara," Aliongea Mercy.

Je una hofu gani katika maishani mwako?