'Single Boy' amewasili,' Harmonize asema baada ya kuwasili Kenya

Muhtasari
  • Mkurugenzi mkuu wa lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide CEO  na msanii wa bongo Tanzani Harmonize amewasili nchini
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo aliwaambia mashabiki wake wa kenya wanapaswa kuwa tayari kwani amewasili
hamo 3
hamo 3

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide CEO  na msanii wa bongo Tanzani Harmonize amewasili nchini.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo aliwaambia mashabiki wake wa kenya wanapaswa kuwa tayari kwani amewasili.

Pia alisisitiza kwamba hana mpenzi na yuko Singo, huku akijisifu na kusema kwamba amekamilisha albamu yake na anapaswa kupumzika.

Harmonize amekuwa Singo baada ya kuachana na Fridah Kajala wiki chache zilizopita, baada ya kuwa pamoja kwa miazi 2.

Msanii huyo aliwasili nchini Jumatatu, baada ya meneja wake Sebastian Ndege kuonekana pia nchini akiwa na mpenzi wake.

"Albamu yangu imekamilika, Nairobi S'ingle boy' amewasili ni wakati wa kupumzika ," Aliandika Harmonize.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki baada ya kufahamu Harmonize amewasili nchini;

blaizemond: MY brother mungu akulinde siku zote

roba_msafi: Nairobi hatutaki maharamia... Rudi mtwara

oseah_wamalengo: ✅ ila tunaomba alltitude iludiwe

cannylovabry: Acha upumbavu wa kuiga iga vitu kutoka kwa Mond, ni ushamba huo