Sipendi wanaume waongo hasa wenye huwakana wake zao-Lilian Muli

Muhtasari
  • Mtangazaji wa runinga ya Citizen Lilian Muli amefichua kwamba hana mume kwa sasa na anafurahia maisha, anazingatia sana biashara na taaluma yake
  • Muli alisema alijifunza mengi kutokana na mahusiano yake ya kimapenzi ambayo aliyapitia awali na kwa sasa hana mpango wa kuwa na mpenzi tena
lilian muli
lilian muli

Mtangazaji wa runinga ya Citizen Lilian Muli amefichua kwamba hana mume kwa sasa na anafurahia maisha, anazingatia sana biashara na taaluma yake.

Muli alisema alijifunza mengi kutokana na mahusiano yake ya kimapenzi ambayo aliyapitia awali na kwa sasa hana mpango wa kuwa na mpenzi tena.

Pia mwanahabari huyo aliweka wazi kwamba hawezi chumbiana na mtu mashuhuri kwa maana kwa kuwa mashuhuri kwake kumempa shinikizo maishani.

LIlian alisema kwamba mwanamuziki ampendayye ni Otile Brown huku akizua mjadala mkali kwenye mitandao hiyo.

Mmoja wa mashabiki wake walimuuliza nini haswa hucukia kutokana kwa wanaume na alikuwa na majibu haya;

"Sipendi wanaume waongo,hasa wale wanwakana wake zao,sema tu ukweli umeoa, kama unachumbia mwanamume alafu baada ya miaka 2 unapata kwamba hana mke tu mmoja bali watatu haiwei,"