JE, WAUNGA MKONO HATUA HII?

Sonko aunga mkono wanawake kuwa na mabwana wengi

Asema kuwa hatua ile itakuwa haki kwani mabibi wa mabwana walio na wapenzi wengi watakuwa wanalipisha kisasi.

Muhtasari

•Sonko adai kuwa tendo la wanawake kuwa na bwana zaidi ya mmoja linafanyika nchini ingawa bado halijakubalika. 

•Asema pia kuwa mwanaume hawezi muacha mke waliyezaa na kuvumilia shida naye kwa sababu ya mpango wa kando

Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi ambaye alitimuliwa,Mike Sonko Mbuvi ameonekana kupendezwa na hatua ya serikali ya Afrika Kusini kuwaruhusu wanawake kuwa na mabwana wengi.

Kupitia jumbe alizochapisha kwenye mitandao yake ya kijamii, Sonko amedai kuwa hivi karibuni wanawake wa Kenya wataruhusiwa kuwa na bwana zaidi ya mmoja. Amesema kuwa hatua ile itakuwa haki kwani mabibi wa mabwana ambao wana wapenzi wengi watakuwa wanalipisha kisasi.

“Hapo nawaunga mkono wanawake. Je wewe fisi unakubali bibi yako aolewe tena na mwanaume mwingine ukiwa nae” Sonko aliandika.

Kwa upande mwingine, Sonko pia amesema kuwa mwanaume hawezi kumuacha bibi aliyepata watoto na kuvumilia shida naye kwa miaka mingikwa sababu ya mpango wa kando.

"Ni heri awaoe wote wawili kama bibi wa kwanza na wa pili. Jambo hilo linampa heshima mke wa kwanza" Sonko alidai