Kuwa maarufu ina bei-Ujumbe wa Zuchu kwa wanaomwendea kinyume

Muhtasari
  • Ujumbe wa Zuchu kwa wanaomwendea kinyume
  • Zuchu ni miongoni mwa wasanii wa lebo ya WCB, ambaye alisajiliwa mwaka jana, huku akivunja rekodi kwa njia ya kipekee
Zuchu-posing-2
Zuchu-posing-2

Zuchu ni miongoni mwa wasanii wa lebo ya WCB, ambaye alisajiliwa mwaka jana, huku akivunja rekodi kwa njia ya kipekee.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemtupia dada yake Diamond Platnumz, Queen Darleen baada ya uvumi kutokea kuwa wamekuwa wakimwendea Zuchu kwa mganga ili asifanikiwe katika kazi yake.

Msanii huyo pia amesajiliwa katika lebo ya WCB, Zuchu akijibu madai hayo alidai kwamba somo ambalo amejifunza katika safari yake ni kuwa kadri anapokuwa ndivyo watu wa karibu naye wanazidi kuwa bandia.

Poa alisema umaarufu una bei yake, Zuchu ametoa nyimbo kadha wa kadha huku asilimia kubwa ya mashabiki wakipenda nyimbo hizo.

"Moja ya Mafunzo makubwa niliyojifunza kutoka kwa safari yangu ni kwamba kadri unavyozidi kukua watu wa karibu nawe wanazidi kuwa bandia

Umaarufu ina bei na katika hali nyingi ni kupoteza watu .Watu unaweza kudhani unajua au unaaminika kuwa wageni wakati wowote Wow Lakinihey Inaitwa maisha halisi," Aliandika Zuchu.