'Mume wangu hakuwa mwendawazimu,'Jacqueline Mengi hatimaye azungumza

Muhtasari
  • Wosia ambao unadaiwa kuandikwa na bilionea marehemu  Reginald Mengi umebatilishwa na Mahakama Kuu jijini Dar Es Salaam
  • Jaji Yose Mlyambina alisema kuwa wosia huo haukutimiza matakwa ya kisheri

Wosia ambao unadaiwa kuandikwa na bilionea marehemu  Reginald Mengi umebatilishwa na Mahakama Kuu jijini Dar Es Salaam.

Jaji Yose Mlyambina alisema kuwa wosia huo haukutimiza matakwa ya kisheria.

Wosia huo pia ulisemwa kuwa haujatiwa muhuri na wakati saini hiyo iliripotiwa kuwa tofauti na kwamba haikushuhudiwa na jamaa yeyote.

Reginald Mengi aliripotiwa kuwa mgonjwa tangu 2016.

Baada ya uamuzi huo, Jacqueline Mengi alishiriki ripoti ya matibabu ya mumewe marehemu akisema kwamba hakuwa mwendawazimu kuzima uvumi na watumiaji wa mitandao ya kijamii.

KUpitia kwenye ukurasa wake wa twitter mjane huyo alikuwa na haya ya kusema;

"Ripoti yake ya matibabu ilidharau Ukweli kwa wale wanaopenda ukweli. Mume wangu hakuwa mwendawazimu, unaweza kusema chochote unachotaka na uchukue kila kitu lakini kwa hili nitamtetea kwenye kitanda changu cha kifo. Dk Kaushik Ranchod wa Afrika Kusini na Dk Anthony Rudd wa Uk wanajua ukweli." Aliandika Jacqueline.

Pia alikanusha madai kwamba mumewe aliandika itabu chake akiwa mwendawazimu, huku akisema yeyote aliyesoma kitabu hicho atashangaa jinsi uvumi unaenea aliandika kitabu hicho kama hayuko timamu