Aliniacha siku ya kulipa mahari yangu-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Lakini kuna wale ambao hufanyiwa vitendo na kujuta maishani mwao kwanini walipatana na wapenzi wao
black-woman-crying-
black-woman-crying-

Uhusiano wako ukifika mahali na mpenzi wako aamue kupeleka mahari nyumbani kwenu wanawake wengi humshukuru Mungu na hata wanaona wamevuka kiwango kimoja hadi kingine.

Lakini kuna wale ambao hufanyiwa vitendo na kujuta maishani mwao kwanini walipatana na wapenzi wao.

Nikiwa katika pilkapilka zangu nilipata na mwanamke aliyefahamika kama Susan ambaye alinisimulia hadithi yake jinsi alitendwa na aliyekuwa mpenzi wake.

Je ukiachwa siku yako ya kulipiwa mahari utafanya nini?

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilikuwa na mpenzi ambaye tulikuwa pamoja kwa miaka 7, tuliamua kuvuka upande huu mwingine, tulifahamiana sana na kutambulishana kwa wazazi weyu

Tulifanya kila tamaduni zote, lakini cha kushangaza ni kuwa, mwanamume huyo siku ya kulipa mahari yangu alitoweka

Alizima simu na kunipa block, ila kitu kilikuwa tayari, hata wazazi wake walikuwa wamefika kwetu bali mwanamume huyo hakufika wala kupeana sababu ya kutofika katika hafla hiyo," Alieleza Susan.

Je mwanamume huyo walipatana tena ama walirudiana baada ya aibu hiyo yote?

"Hatukuwasiliana kwa muda wa mwezi mmoja, lakini niliendelea na maisha yangu na pia yeye aliendelea na maisha yakke na akaoa, hajwahi nopa sababu ya kuniacha nami sijawahi kusumbuka kumuuliza kwani ni uchungu sana kukumbuka yale maneno mengi yalisemwa

Kusema kweli katika kila mapito kuna somo ambalo mtu anapaswa kujifunza."