"Alishtuka nilipomwambia kuwa tunadate" Bahati azungumzia safari yake ya mapenzi

Mwanamuziki wa nyimbo za injili, Kevin Bahati, awashauri vijana wasisubiri sana kutangaza mapenzi yao

Muhtasari

•Bahati amekiri kuwa tukio la kutangaza mpenzi wake lilimfanya kupoteza tuzo la Groove

•Awashauri vijana wasisubirie sana kutangaza mapenzi

Bahati na Diana
Bahati na Diana
Image: Hisani

Mwanamuziki wa nyimbo za injili, Kelvin Kioko, almaarufu kama Bahati amefunguka kuhusu safari ya mapenzi yake na mpenzi wake Diana Marua.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bahati amekiri kuwa alimtangaza Diana kuwa wake wiki tano tu baada ya kujuana tendo ambalo lilimshtua sana Diana kwani ilitendeka haraka.

Ilihisi haraka sana kwake kwani alitarajia nilifanye jambo ngumu sana, lakini mimi kama kijana wa ghetto mnajua vile tufanyavyo” Bahati aliandika.

Ameendelea kueleza kuwa aliagiza kupatana na wazazi wake Diana baada ya miezi tano ya kuchumbiana. Tukio ambalo lilimfanya yeye kupoteza tuzo la Groove.

Miezi tano tu? Naam, mbona nisubiri hadi milele ikiwa nishajua kuwa ni yeye?? Nakumbuka siku ile ndipo nilipomtangaza kama mshirika mwenza wa maombi, tendo ambalo lilinifanya kutimuliwa kwenye tuzo la groove na jopo, habari ya siku ingine lakini”  

Bahati ameonekana kusherehekea ndoa yake ya miaka tano na Diana huku akijivunia kubarikiwa kwao na watoto watano.

Bado sijaelewa tunavyoweza kuwatimizia matakwa yao lakini nawaahididd kuwa Mungu hajawahi ruhusu watoto wale kukosa” Diana amesisitiza.

Mwanamuziki yule amewasihi vijana wasisubiri sana kwani wakati hauwasubiri.

Kama unaweza jihusisha kwenye mapenzi, basi fanya mara moja mengine utakuja kusoma baadae. Hakuna kitu kama mke ama mume kamili , kama unaamini kuwa yeye ndiye sawa kutumikia wakati wako naye, muunde hadi aafikie mapenzi yako” Bahati alisema.