'Haina haja yakulalamika,'Alikiba amwambia Diamond baada ya kuisuta Forbes

Muhtasari
  • Alikiba ampa Diamond vijembe baada ya kuisuta Forbes
  • Alikiba kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter alimsihi Diamond awache kulalamika kwani waliomuweka kwenye orodha hiyo wana akili ndefu
ali-kiba
ali-kiba

Ugomvi kati ya msanii wa bongo Alikiba na staa wa bongo Diamond Platnumz umeshuhudiwa kwa muda sasa na mashabiki wao.

Siku ya JUmatano Diamond Platnumz kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliisuta kampuni ya Forbes kwa kumuweka kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.

Mwanamuziki huyo tokea Tanzania aliwasihi Forbes kufanya utafiti dhabiti kabla ya kuweka jina lake kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.

Baada ya Diamond kusuta kampuni hiyo, Alikiba kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter alimsihi Diamond awache kulalamika kwani waliomuweka kwenye orodha hiyo wana akili ndefu.

"Sadala nisikilize ,kati ya hao watu ambao wewe unajidanganya kuwa Ni wenzako , na kudanganya watu wenye ufupi wa akili .hakuna hata mmoja ametanga ana hela akaandikwa FB. haina haja yakulalamika sisi ukituambia kama unahela tunaamini inatosha ila wale wana akili ndefu (mediocre),"

Ni ujumbe ambao ulimweka Alikiba pahali pabaya na mashabiki baada ya mashabiki wake Diamond kumkashifu kwa maneno au usemi wake.