'Pesa isiwai kufanya ukamdharau mtu,'Muigizaji Maria awashauri mashabiki

Muhtasari
  • Muigizaji Maria awashauri mashabiki  
  • Siku baada ya siku muigizaji huyo alitia bidii na hata kupata kazi ya ubalozi katika kampuni ya Noodles
  • Pia amekuwa akiwaburudisha mashabiki wake kupitia kwenye mitandao ya kijamii, kwa mambo kadha wa kadha

Muigizaji Yasmeen Saiedi almaarufu Maria alifahamika sana kutokana na uigizaji wake katika kipindi kilichokuwa kinapeperushwa katika runinga ya Citizen kinachofahamika kama 'Maria'.

Siku baada ya siku muigizaji huyo alitia bidii na hata kupata kazi ya ubalozi katika kampuni ya Noodles.

Pia amekuwa akiwaburudisha mashabiki wake kupitia kwenye mitandao ya kijamii, kwa mambo kadha wa kadha.

Watu wana tabia ya kuwadharau wenzio baada ya kupata pesa au kwa lugha ya mtaa baada ya 'kuomoka'.

Lakini kulingana na Maria ukiwa na pesa hupaswi kumdaharau mtu na kazi yake kwani hujui ya kesho.

Ni ujumbe ambao mashabiki walimpingeza Maria kwa kuzungumza ukweli.

"Pesa isiwai kufanya ukamdharau mtu na kazi yake!๐Ÿ•Š," Aliandika Maria.

Haya hapa maoni ya mashabiki wake;

hefnerkenya: Naona unaficha mimba ya Maria wa kitaaa the character eeeeeh๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

lydiamwikz87: Mwenye maskio na askie

eddieoliech: Mawaidha na Bi Yasmin

tony_mwirigi: Maneno ya Busara kutoka Kwa Binti Wa Kitaaa๐Ÿ”ฅ

gracenaisola: Kweli maria Bora anapata rizki yake ,, inshallah

hefnerkenya: Yasmeen nkuoneaje.....kesho njoo miale ukunywe kahawa๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚