Nyota Ndogo afunga safari hadi Denmark kumsuta mumewe

83532576_627204834703118_8454513908795708531_n
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n

Baada ya utani wake kuharibu uhusiano wake na mumewe, Nyota ndogo sasa ameamua kusafiri hadi Denmark kumsuta Bw. Henning Nielsen.

Katika mahojiano juma kadhaa zilizopita Nyota Ndogo alisema baadhi ya wanamitandao walimwambia kwamba mumewe alikuwa anatafuta sababu ya kumuacha.

Hata hivyo, licha ya mumewe kusitisha mawasiliano kati yao, aliapa kusafiri hadi Denmark ili kujaribu kusuluhisha mambo kati yao.

"Nimekuwa nikizungumza na mwanawe, lakini mwanawe akimwambia kuhusu jina langu anakata simu

Amenipa block kila mahali, napanga kuenda Denmark ilitusuhishe mambo pamoja akinifukuza ni sawa pia.

Sikubaliani na maoni ya mashabiki kwamba alikuwa anatafuta sababu ya kuniacha, kwa maana amenijengea nyumbani saba na hawezi kuniacha," Alisema Nyota akiwa kwenye mahojiano.

Ni dhahiri kuwa msanii huyo kutoka mkoa wa Pwani hakuwa na utani na hii leo amechapisha picha akiwa amefunganya virago akielekea Denmark.

Nyota aliandika,

Asipokuja mfate. Don’t giveup on your love.. Nikifukuzwa pia ntawaambia