Mungu alikuwa mwaminifu-Mkewe Guardian Angel anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Mke wa Guardian Angel Esther Musila anatimiza miaka 51 leo lakini  anawakumbusha watu kuwa ana miaka 21 tu na uzoefu wa miaka 30
  • Pia alikumbuka vile marafiki walimkimbia mambo yalipobadilika
Guardian Angel na Esther Musila
Guardian Angel na Esther Musila
Image: Instagram

Mke wa Guardian Angel Esther Musila anatimiza miaka 51 leo lakini  anawakumbusha watu kuwa ana miaka 21 tu na uzoefu wa miaka 30.

Pia alikumbuka vile marafiki walimkimbia mambo yalipobadilika.

"Mungu ananiambia leo,Ulishikilia wakati wa nyakati ngumu zaidi. Nilikupa nguvu kuhakikisha kuwa wakati mwingine hata sikujua ni mimi

Wakati mambo yalibadilika kwako wengi walikuacha na kukuandikia barua. Lakini ni wewe tu ulivumilia dhoruba .. ulikua katika dhoruba

Wewe ni tofauti. Sikukuumbia uweze kutoshea ... nimekuumba ujulikane. Sasa niko karibu kubariki uaminifu wako. Niko karibu kukupeleka kwenye viwango ambavyo hata haukufikiria vingewezekana ," Aliandika Musila.

Pia alimshukuru Mungu kwa kuwa naye nyakati zake ngumu, na kumshika mkono, pia aliwashukuru wanawe kwa upendo ambao wamemuonyesha na kumshika mkono.

"Ninaposherehekea mwaka mwingine, ninataka kumshukuru Mungu kwa maisha haya ambayo sisi huwa tunayachukulia kawaida

Mengi yametokea katika mwaka uliopita lakini Mungu alikuwa mwaminifu njia yote. Kwa uzoefu wote, nilitoka 💪

Mwaka huu uliopita umekuwa na raha kusema kidogo. Nimejifunza kuishi, kuishi kwa ajili YANGU, na ninapenda sehemu hii ya safari yangu na mtu wa kushangaza sana Mungu amemleta kwenye maisha yangu, Mfalme wangu, G wangu,"

KUtoka kwetu wanajambo heri ya kuzaliwa Esther Musila.