- Kambua Atoa kibao kipya Baada ya Kumpoteza mwanawe
Msanii wa nyimbo za injili na mtangazaji maarufu Kambua, alirejea mitandaoni siku ya Ijumaa baada ya kuchukua likizo kwa miezi mitatu.
Aliwashukuru mashabiki wake kwa kumuombea alipopitia magumu, bali na hayo hakuwashukuru mashabiki bali alitoa kibao cha shukrani kwa Mungu.
Kambua amesema wimbo huo mpya ameotoa wakati wa dhiki na faraja kwa wakati mmoja.
" Shukrani ni wimbo ambao niliotoa wakati wa huzuni mwingi ila pia kwa shukrani kwa Mungu wangu
Hali hizi mbili kwa sasa zinaambatana na najua Mungu anabaki kuwa Mungu kwa kila ambacho ametufanyia
Mungu huwa anatufaruji na kutuahidi kutembea nasi katika bonde la mauti, kwa hivyo, anaponiunua na kunifariji, hebu na pia akutendee pia wewe, Mungu anajua kuwafidia wanawe, najua hawezi kukuacha, Mungu ni mkuu," Kambua Alisema.
Mashabiki walimkaribsha msanii huyo, kwa furaha huku wengi wakikiri walikuwa wamempeza sana.