Achaneni na watu waishi maisha yao',Akothee asema baada ya Elsa Majimbo kusema hatamani kurudi Kenya

Muhtasari
  • Mchekeshaji Mkenya Elsa Majimbo amefunua sababu za kwanini alihama Kenya na asingependa kurudi
  • Kulingana na Elsa, watu wa Nairobi wamekuwa wakimkejeli kwa muda sasa
Elsa Majimbo
Image: Maktaba

Mchekeshaji Mkenya Elsa Majimbo amefunua sababu za kwanini alihama Kenya na asingependa kurudi.

Kulingana na Elsa, watu wa Nairobi wamekuwa wakimkejeli kwa muda sasa.

Kijana wa miaka 19 ambaye amekuwa akiishi Dubai alisema kuwa angependa kwenda Afrika Kusini kuliko kukaa au kurudi Nairobi.

Akiwwa kwenye mahojiano Majimbo Alisema kuwa anaweza kushughulikia maoni mabaya lakini sio watu wanaomhurumia.

Ni kitendo ambacho msanii Akothee amegadhabishwa nacho huku aisema hawezi hama kenya, kwani watu wakimtusi pia atawatusi.

Pia aliwasihi wanamitandao wanaojiona kwamba wao ni warembo kupindukia, wawacche watu waishi maisha yao.

"Mimi Sihami hii kenya ,tunangangana tu hapa , hata waniitukane Aje, wakinitukana,nawatukana wakinipenda nawapenda,

Mimi siwezi wachia mtu utamu ya kenya sababu ya mtu anapangusa matako na oboke No Wayniliwaambia watoto wangu hayo hayo,mtu. Akikutusi online,jiachilie,matusi kwa gunia walishwe. wasichana na wavulana wenye sura nzuri na  wazungu wamitandao ya kijamii wanadhani kwamba wana haki kuliko wasichana wenye ngozi nyeusi

Hello achaneni na watu waishi maisha yao.ni huzuni na huruma nyingi kuwasukuma wasichan wadogo kufikiria kuwa weusi ni sura mbaya Nkt." Aliandika Akothee.