YEYE NI NANI?

"Yeye ni nani, amewafanyia nini?" Akothee akiri kutomjua Embarambamba

Akothee alisema kuwa Wakenya wana mazoea sana ya kumtumia yeyote aliyewakosea.

Muhtasari

•Shabiki mmoja alitengeneza chapisho la kumtania Akothee kuwa aliwanga anajitayarisha kupatana na Embarambamba

•Akothee alisema kuwa alikuja kuskia kuhusu Embarambamba kutokana na jumbe za mashabiki kwenye ukurasa wake.

Akothee akifanya tizi
Akothee akifanya tizi
Image: Instagram

Mwanamuziki na mwanabiashara mashuhuri, Esther Akoth amekiri kuwa amekuja kumsikia Embarambamba kutokana na jumbe za mashabiki kwenye ukurasa wake.

Akothee amesema kuwa huwa hatazami runinga na kuwataka mashabiki kumuelezea Embarambamba ni nani.

"Nimekuja kuskia kuhusu Embarambamba kupitia jumbe mnazoandika hapa. Yeye ni nani? mnisamehe huwa sitazami runinga. Ningetaka kujua yeye ni nani haswa na amefanya nini? Akothee aliuliza kupitia mtandao wa Instagram.

Hii ni baada ya shabiki mmoja kutengeneza chapisho la kumtania Akothee amaarufu kama 'memes' akisema kuwa Akothee anajitayarisha kumwona Embarambamba.

Mwanzilishi huyo wa Akothee safaris alisema kuwa Wakenya wana mazoea ya kumtumia kila aliyewakosea.

"Najua kila mwenye amewakosea Wakenya huwa natumiwa Akothee. Embarambamba amewafanya nini" Akothee alitaka kujua.

Embarambama amekuwa akienea mitandaoni kwa muda kutokana na sarakasi nyingi anazofanya kwa nyimbo zake na drama zinazomkumba. Wiki iliyopita video mbili zilisambazwa mitandaoni ambapo alionekana akishirika kwenye densi isiyo ya kimaadali na mashabiki.