'Siwezi unga mkono ujinga,'Shakilla awakejeli wasanii wakenya

Muhtasari
  • Shakilla ashambulia wasanii wa kenya huku akiunga mkono Diamond na lebo ya Wasafi
Shakilla

Mwanasosholaiti Shakilla kupitia kwenye mitandao yake ya instagram aliwakejelu wasanii wa humu nchini kwa ujumla uku akiunga Diamond Platnumz katika Tamasha ya BET Awards.

KUlingana na mwanasosholaiti huyo hawezi akaunga mkono ujinga.

Diamond Platbumz katika Tamsha ya BET aatashindana na wasanii kama vile,Davido, Wizzkid miongoni mwa wengine.

Ni orodha ambayo iliwafanya wasanii wa Tanzania kutambulika, kulingana n Shakilla kuchaguliwa kwwake Diamond kumethibitisha kwamba wasanii wa kenya hawayuko makini na kazi yao.

Alijiuliza ni wapi Wakenya wamekosea kwani wasanii wa Kenya walidaiwa kucheza muziki wa kilema, kwa jina la mpango wa PlayKE.

"Nashindwa ni wapi wakenya walikosea,wasaii hawa wote wanaimba tu nyimbo kwa jina la mpango wa PlayKE

Na ndio maana wasafi itazidi kuvuma na kuongoza, siweezi unga mkono ujinga, niite Shakilla kutoka kwa ncchi nyingine lakini sio kenya pooooooo!!!MATHOGOTHANIO," Aliandika Shakilla.