Hatimaye mumewe Nyota Ndogo ajibu jumbe zake

Mwanamuziki huyo wa takriban miaka 40 pia amefurahia kuona kuwa mumewe bado anatumia picha yake kama picha yake ya wasifu, WhatsApp

Muhtasari

•Kwa muda sasa, wawili hao hawajakuwa katika hali ya kuelewana huku msanii huyo kutoka Pwani akitumia mitandao ya kijamii kujaribu kumsihi mumewe kumrudia.

Nyota Ndogo na mume wake mzungu
Nyota Ndogo na mume wake mzungu
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki Nyota Ndogo ameonekana mwenye bashasha baada ya mumewe kusoma na kujibu ujumbe wake kwa mara ya kwanza tangu amuache.

Kwa muda sasa, wawili hao hawajakuwa katika hali ya kuelewana huku msanii huyo kutoka Pwani akitumia mitandao ya kijamii kujaribu kumsihi mumewe kumrudia.

Nyota Ndogo amechapisha picha aina ya screenshot inayoonyesha mazungumzo mafupi kati ya wawili hao.

Nyota Ndogo: Hallow (10.34 PM)

Nyota Ndogo: Hi (10.34PM)

Henning: Ninakukosa rohoni sana mke wangu (10.36PM)

Baada ya kupokea jibu kwenye mtandao wa WhatsApp, msanii huyo alikimbia kusherehekea furaha yake na mashabiki kwenye mtandao wa Instagram.

"Jamani amkeni Leo nakesha nimeblue tikiwa na nikaitwa mke amenimiss jamani amkeni. Nashindwa la kujibu naanzaje kujibu jamani silali leo ntaangalia tu huu ujumbe" aliandika nyota huyo wa kibao 'watu na viatu' kwenye mtandao wa Instagram.

Mwanamuziki huyo wa takriban miaka 40 pia amefurahishwa kuona kuwa mumewe ambaye amenakili nambari yake kama 'Sabuni ya moyo wangu' bado anatumia picha yake kama picha ya wasifu.

Mashabiki wameendelea kutoa hisia tofauti