Lala salama!Msanii Janet Otieno ampoteza baba yake

Muhtasari
  • Msanii Janet Otieno ampoteza baba yake
  • Alitangaza habari hizo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, huku akiwaomba mashabiki wawaeke kwa maombi hasa wakati huu mgumu
Msanii Janet Otieno
Image: Maktaba

Msanii wa nyimbo za injili Janet Otieno, yuko kwenye aombolezi baada ya kumpoteza baba yake mzazi.

Alitangaza habari hizo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, huku akiwaomba mashabiki wawaeke kwa maombi hasa wakati huu mgumu.

"Kumpoteza mzazi sio jambo rahisi, moyo wangu umevunjika kwa vipande, hamna kitu ambacho kingeniandaa kwa uchungu ambao napitia sasa

Lala salama papa, milele utakuwa kwenye iouo yetu, tafadhali tukumbukeni kwa maombi wakati huu mgumu tunapoomboleza," Aliandika Janet.

Hizi hapa jumbe za mashabiki wakimtia moyo msanii huyo;

massawejapanni: Oooooooh😢😢😢😢😢Take heart dear

pierramakenaofficial: Pole sana my dear... hugs of prayers

joyceomondi: So sorry siz. May the Lord comfort you deeply during this time 🙏🏾❤️

weezdom254: Pole Sana Mum🙏 my condolences

sandra_dacha: Pole Sana dear. Tuko pamoja

mylee_staicey: Sorry Mum,it is well😢My deepest condolencesMay He RIP