POLENI MOH NA KYM

Mandugu wacheza santuri, DJ Moh na DJ KYM waomboleza baba yao

Mandugu hao walifanya tamasha ya kumpa heshima baba yao siku ya Alhamisi.

Muhtasari

•Siku ya Alhamisi, Moh na Kym ambao ni mandugu walitangaza kuaga kwa baba yao mzazi kupitia mtandao wa Instagram. Hata hivyo, hawakueleza kilichosababisha maafa hayo.

•Wawili hao walijitosa kwenye sanaa ya ucheza santuri takriban miaka kumi na tano iliyopita na wamepata umaarufu mkubwa sana nchini kutokana na michezo yao.

Dj Moh na DJ KYM NICKDEE
Dj Moh na DJ KYM NICKDEE
Image: Instagram

Wacheza santuri maarufu Nicholas Mugo almaarufu kama DJ Moh Spice na David Mwangi almaarufu kama DJ Kym NickDee wanaomboleza kifo cha baba yao.

Siku ya Alhamisi, Moh na Kym ambao ni mandugu walitangaza kuaga kwa baba yao mzazi kupitia mtandao wa Instagram. Hata hivyo, hawakueleza kilichosababisha maafa hayo.

Wawili hao walijitosa kwenye sanaa ya ucheza santuri takriban miaka kumi na tano iliyopita na wamepata umaarufu mkubwa sana nchini kutokana na michezo yao.

Walianzisha kampuni ya burudani kwa jina NickDee, kifupi cha Nicholas na David.

Moh anatambulika sana kwa kucheza ngoma aina ya reggea ilhali Kym anapendelea kucheza nyimbo aina ya Hiphop.

Kwa sasa Moh anacheza santuri katika runinga ya NTV kwenye kipindi cha Jam Down naye Kym anacheza katika stesheni ya Kiss TV.

Wakenya wengi ikiwemo wasanii na mashabiki wameendelea kutoa rambirambi zao kwenye kurasa za Instagram za wawili hao.

Moh na KYM walifanya tamasha ya kumpa heshima baba yao siku ya Alhamisi.