MNIKOME!-AKOTHEE

Akothee afokea wanaotumia jina na nambari yake kujigamba

Amewaonya wanaume wanaotumia jina na nambari yake ya simu kutishia mabibi zao huku akiwaambia pia yeye hakuna vile atawasaidia na wakiachwa wajipange.

Muhtasari

•Msanii huyo mwenye umri wa miaka 41 pia ameeleza kutoridhishwa na baadhi ya watu wanaopatia watu asiojua simu ili kuzungumza naye wakidai kuwa ni mashabiki.

•Amesema kuwa usiri wake ni muhimu sana.

Akothee
Akothee
Image: Instagram

Mwanamuziki Esther Akoth akmaarufu kama Akothee amekashifu watu ambao wanatumia jina lake kujinata.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee ametangaza kuwa atakatiza mawasiliano na wanaume wote ambao wanatumia jina lake kujigamba kwa mabibi wao, marafiki na wenzao.

"Nitakomesha wanaume wanaotumia jina langu kujinata kwa mabibi zao, marafiki na wenzao. Mahali ujinga wenu wenu unafika basi hapo ndipo wangu waanza. tumbafu hii. Ujinga wa kunitumia kama chombo cha kutishia wake zenu itakoma!" Akothee aliandika.

Msanii huyo ambaye pia ni mwanabiashara mashuhuri amesema kuwa hapo awali aliogopa marafiki wanawake kwani wao ndio walikuwa na tabia kama zile ila amesikitika kuona kuwa baadhi ya marafiki wake wanaume pia wamechukulia tabia hizo

."Hata wanaume wamekuwa wajinga sana, ati Akothee ananitaka, wewe nikikutaka si utatimua huyo bibi uhamie Rongo ama ikulu?! Haya maisha bandia yanafanya maisha kuwa tofauti sana na magumu. Dunia yangu inakuwa ndogo" Akothee alieleza.

Amewaonya wanaume wanaotumia jina na nambari yake ya simu kutishia mabibi zao huku akiwaambia pia yeye hakuna vile atawasaidia na wakiachwa wajipange.

"Ile siku mkeo atanivamia na mambo ya kishenzi, basi nitafichua familia yako mtandaoni" Akothee aliwaeleza wanaume wenye tabia hizo.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 41 pia ameeleza kutoridhishwa na baadhi ya watu wanaopatia watu asiojua simu ili kuzungumza naye wakidai kuwa ni mashabiki.

"Wajua pia sisi wasanii ni binadamu pia na tunahitaji kutangamana na watu wengine mara kwa mara. Na tafadhali muache kupatia watu sijui simu zenu eti tuongee nao kwa kuwa wananipenda! alafu?" Akothee aliandika.

Ameeleza kuwa huwa hapendi simu kama hizo na huwa anakata mara moja.

"Sio eti mimi ni mjeuri ila lazima nilinde hadhi yangu. Mbona wataka nizungumze na watu nisiowajua? unataka nihusiane nao aje? Je wajua ilivyo ngumu kuanzisha mazungumzo na mtu ambaye humjui na hamjawahi patana??" Aliendelea kusema.

Amesema kuwa usiri wake ni muhimu sana.