JE, MAGIX ENGA AKO SALAMA?

Wasiwasi baada ya mwanamuziki kudai kuwa angefariki Ijumaa usiku

Wakenya wengi ikiwemo wasanii wenzake wamefanya juhudi za kuwasiliana na Magix Enga ila hakuna aliyetangaza kufanikiwa kumfikia

Muhtasari

•King Kaka na Kristoff ni baadhi ya wasanii ambao wameeleza kuwa juhudi za kumfikia Magix Enga hazijafua dafu.

Magix Enga
Magix Enga
Image: Instagram

Hali ya wasiwasi imetanda katika mtandao wa Instagram baada ya mwanamuziki na mtengezaji wa nyimbo Magix Enga kuchapisha ujumbe kuwa angefariki usiku wa kuamkia Jumamosi.

Mwanamuziki huyo wa nyimbo aina ya gengetone alichapisha ujumbe "I'm gonna die tonight"(nitafariki usiku wa leo) mida ya saa nne unusu usiku.

Aliendelea kusema kuwa angepenza kila mtu.

'"I'm going to miss everyone"(Nitawapeza nyote)"

Haijabainika wazi kilichomfanya Enga kuchapisha ujumbe huo ambao umeshtua Wakenya wengi huku wengine wakibashiri kuwa huenda ni huzuni.

Wakenya wengi ikiwemo wasanii wenzake wamefanya juhudi za kuwasiliana na mwanamuziki huyo ila hakuna aliyetangaza kufanikiwa kumfikia.

Jumbe za King Kaka na Kristoff
Jumbe za King Kaka na Kristoff

King Kaka na Kristoff ni baadhi ya wasanii ambao wameeleza kuwa juhudi za kumfikia Magix Enga hazijafua dafu.