Hongera!Bendi ya Sauti Sol hatimaye yampongeza msanii Diamond Platnumz

Muhtasari
  • Bendi ya Sauti Sol  hatimaye yampongeza msanii Diamond Platnumz
sauti.sol
sauti.sol

Bendi ya humu nchini ya Sauti Sol wamejiunga na orodha ya wasanii ambao wanaunga mkono uteuzi wa msanii wa Tanzania Diamond Platnumz kwenye tuzo za BET.

Diamond ameteuliwa kwenye Tuzo za BET 2021 kama msanii pekee wa Afrika Mashariki chini ya kitengo, Best International Act.

Wengine ambao wametajwa katika kitengo cha Sheria Bora ya Kimataifa ni pamoja na; Aya Nakamura,Buena Boy,Wuzkid miongo mwa wengine.

Naam, Bendi ya Kenya Sauti Sol wamempongeza bosi wa WCB na kuwaomba mashabiki wao kusaidia katika kupiga kura ili Diamond aweze kushinda tuzo hiyo.

Baadhi ya watu na wanamitandao walipinga uteuzi huo na hata kukejeli kampuni ya BET.

Kupitia kwenye ukurasa wao wa instagram bendi hiyo ilikuwa na haya ya kusema kuhusu uteuzi wake staa Diamond.

"Hongera sana kwa uteuzi wako ndugu yetu, wacha tupate tuzo hiyo @Diamondplatnumz," Ilisema.