'Nahitaji helmet,'Msanii Bien asema baada ya madai wanaume wenye vichwa vya upara wamo hatarini

Muhtasari
  • Mwimbaji Bien Aime Baraza ameshtuka baada ya ripoti kwamba wanaume wenye vichwa vipara wanawindwa ili kutumika kwa mila ya uchawi
Bien
Image: Maktaba

Mwimbaji Bien Aime Baraza ameshtuka baada ya ripoti kwamba wanaume wenye vichwa vipara wanawindwa ili kutumika kwa mila ya uchawi.

Kulingana na ripoti ya BBC, wanaume wenye upara wamekuwa wakilengwa nchini Msumbiji kwani wanafikiriwa kuwa na dhahabu.

Watu watano wameuawa na watu wakidhani kwamba kuna dhahabu ndani ya vichwa vyao. Mmoja wao viungo vyao vimetolewa nje

Washukiwa wamekamatwa na wamewaambia polisi kwamba viungo vya watu wenye upara na vinatumika kwa vitendo vya ushirikina nchini Tanzania. "Mwandishi wa BBC Swahili alisema.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alielelza hofu yake na kudai kwamba anahitaji walinzi 10 kwa ajili ya habari hizo.

"Nahitaji walinzi karibu kumi,mabawa kadhaa na helmet," Aliandika Bien.

Hizi hapa hisia za mashabiki  baada ya ujumbe wake msanii huyo wa bendi ya Sauti sol.

jackyvike: 😂😂😂Ah! Lazima ingekua Tz

joydoreenbiira: Is it this serious 😃

nicki_bigfish: Sema kime umana!😂😂

felixjay_z: Akuna venye bien ako na gold ndani ya kichwa ! Mnajua vizuri sana ni bhangi safi 😅

1omogambi: Wanenyofolewa viungo 😭😂😂😂😂😂😂😂😂😂