JE, NI KWELI?

"Ni heri kufanya kazi na wanaume mashoga" Huddah asema

Mwanasosholaiti Huddah Monroe amesema kuwa ni rahisi kufanya kazi na mashoga kwani hawapatwi na fikra za shughuli za kitandani wanapokuwa kwenye mazingira ya kikazi na wanawake.

Muhtasari

•Mwanasosholaiti na ambaye pia ni mwanabiashara amesema kuwa ni ngumu sana kwa mwanamke kufanya biashara katika ulimwengu unaotawalwa na wanaume.

•Huddah amepeana mfano wa wakati alikuwa anatoa wasilisho kwenye chumba kilichokuwa na wanaume 12 na mwanamke mmoja huku akieleza kuwa wanaume hao hawakuelewa chochote.

Huddah Monroe
Huddah Monroe
Image: Instagram

Mwasosholaiti mashuhuri Huddah Monroe amezungumzia masaibu anayopitia wakati anafanya kazi na wanaume.

Mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 29 ameeleza namna wanaume huwa hawakuwi makini anapozungumza mbele yao.

"Huwa najaribu kuwa na heshima ya kikazi kila ninapofanya kazi na wanaume ila wanachoona ni uchi wangu ukiwa umechorwa kwenye uso! Vituko gani hizi? SMH" Huddah aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Huddah alieleza kuwa ni rahisi kufanya kazi na mashoga kwani hawapatwi na fikra za shughuli za kitandani wanapokuwa kwenye mazingira ya kikazi na wanawake.

"Uzuri tuko na mashoga ambao ni wabunifu na hawana vituko na hawana tamaa ya kulala nami. Ni rahisi sana kufanya kazi nao" Huddah alisema.

Huddah amepeana mfano wa  wakati alikuwa anatoa wasilisho kwenye chumba kilichokuwa na wanaume 12 na mwanamke mmoja huku akieleza kuwa wanaume hao hawakuelewa chochote.

"Kwa mfano kuna wasilisho ambalo natamani sana ningerekodi. Chumba kilikuwa na wanaume 12 na mwanamke mmoja tu. Nilifanya wasilisho langu kwa muda wa dakika 30 na wanaume wale hawakuelewa chochote. Walikuwa kwenye dunia ya ndoto." Alisema Huddah.

Mwanasosholaiti na ambaye pia ni mwanabiashara amesema kuwa ni ngumu sana kwa mwanamke kufanya biashara katika ulimwengu unaotawalwa na wanaume.

"Ni lazima uwe jasiri. Nawapongeza wanawake wote ambao wamefanikiwa tayari. Mnanipa motisha" Aliendelea kusema.

Huddah ameeleza kuwa angependa kuwa mwanamke wa kuigwa na wasichana wengine.

"Nataka niwe mwanamke ambaye wasichana watakuja nyumbani na waseme, nataka kuwa kama Hudda! Hakuna kingine! Tazamia kuhamasisha wengine" Huddah alisema

Mwanamuziki Akothee amemuunga mkono katika suala hilo huku akisema kuwa pia naye anashuhudia matatizo anapofanya kazi na wanaume.

"Nakupongeza Huddah, mashoga ndio bora, ila wamejaa udaku, wengine hawa hisia imara wanalia  sana. Hakuna haki ya mwanamke katika haya maisha" Akothee alisema.