BURIANI BABA JOYCE

Safiri salama! Mwanamuziki Joyce Omondi aomboleza babake

Akitangaza kuaga kwa babake kupitia mtandao wa Instagram, msanii huyo ambaye ni mke wa mwanahabari mashuhuri wa runinga ya Citizen amemsifia babake huku akijivunia kuwa binti ya 'baba wa ajabu'

Muhtasari

•Wakenya wengi ikiwemo wasanii na wanahabari mashuhuri ikiwemo Victoria Rubadiri, Emmy Kosgei, Yvonne Okwara, Kirigo Ngarua, Terryanne Chebet na wengineo wametuma jumbe zao za rambirambi.

•"Kuna shimo kubwa lililoachwa moyoni mwangu kwa kuwa Baba wa Mbinguni uliyenifunza kupenda na kuhudumia amekuita nyumbani kwake. Ni Mungu tu anayeweza kujaza nafasi uliyoacha kwa kuwa urithi wako ni mkubwa kuliko maisha" Omondi aliandika.

Joyce Omondi na Baba yake
Joyce Omondi na Baba yake
Image: Instagram

Mwanamuziki wa nyimbo za injili, Joyce Omondi anaomboleza kifo cha baba yake.

Akitangaza kuaga kwa babake kupitia mtandao wa Instagram, msanii huyo ambaye ni mke wa mwanahabari mashuhuri wa runinga ya Citizen, Waihiga Mwaura, amemsifia babake huku akijivunia kuwa binti ya 'baba wa ajabu'

"Kati mwa mafanikio makubwa maishani mwangu ni fadhila ya kuwa binti ya mwanaume huyu wa ajabu. Yeye nii kila kitu ambacho ningeombea na kutamani kwa baba. Mapenzi makubwa, utunzaji, uungaji mkono na ulinzi ulionipa ni wachache mno waliobahatika kupata." Omondi aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

"Kuna shimo kubwa lililoachwa moyoni mwangu kwa kuwa Baba wa Mbinguni uliyenifunza kupenda na kuhudumia amekuita nyumbani kwake. Ni Mungu tu anayeweza kujaza nafasi uliyoacha kwa kuwa urithi wako ni mkubwa kuliko maisha" Omondi aliandika.

 

Wakenya wengi ikiwemo wasanii na wanahabari mashuhuri ikiwemo Victoria Rubadiri, Emmy Kosgei, Yvonne Okwara, Kirigo Ngarua, Terryanne Chebet na wengineo wametuma jumbe zao za rambirambi.

jumbe za rambirambi
jumbe za rambirambi
Image: Instagram
jumbe za rambirambi
jumbe za rambirambi
Image: Instagram

Kutoka Radio Jambo, tunaombea familia ya Omondi faraja na Mungu alaze moyo wa Baba Joyce mahala pema peponi