'Hawakuelewa,' Corazon Kwamboka afichua aliwapoteza marafiki baada ya kujifungua

Muhtasari
  • Corazon Kwamboa afichua aliwapoteza marafiki baada ya kujifungua
corazon
corazon

Mwanasosholaiti Corazon Kwamboka kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefichua kwamba aliwapoteza marafiki wengi baada ya kujifungua.

Mwanasosholaiti huyo alijifungua mwishoni mwa mwaka jana.

Kulingana na Corazon baadhi ya marafiki wake hawakuelewa kwamba maisha yake yamebadilika.

Pia alisema kulea kumebadilisha maisha yake kwenye mitandao ya kijamii.

"Kuwa mama nilipoteza marafiki wengi wasio na watoto. Hawakuweza kuelewa maisha yangu mapya

Hakuna mtu anayekuambia jinsi maisha yako ya kijamii yatakavyobadilika kwa kasi😂. Kwa hivyo kila wakati mmoja mbali na mtoto wangu wa thamani huchukuliwa kwa shukrani nyingi

Ninavaa vizuri, ninaonyesha mapaja yangu mazito, mapambo (mmmhh, hapa bado natafuta msaada) na kujifurahisha kwa kiwango cha juu." Aliandika Corazon.