Wakenya mashuhuri ambao wako na watoto pamoja licha ya kutokuwa kwa ndoa

Soma orodha ya Wakenya mashuhuri ambao hawako kwenye uhusiano na waliwahi pata watoto pamoja

Muhtasari

•Gumzo kubwa iliibuka mwezi Mei miongoni mwa Wakenya baada ya kufichuliwa kuwa  wacheshi Hamo na Jemutai wako na watoto wawili pamoja

Jemutai, Erick Omondi, Brenda Wairimu, King Kaka
Jemutai, Erick Omondi, Brenda Wairimu, King Kaka

Eric Omondi na  Jackie Maribe

Mcheshi Eric Omondi na aliyekuwa mtangazaji wa stesheni ya Citizen, Jackie Maribe wako na mvulana mmoja kwa jina Zahari.

Maribe aliweka jambo hilo wazi wakati kijana huyo wa miaka saba alikuwa anahitimu kuingia darasa la  kwanza  mwaka wa 2019.

“Familia yaja mbele. Siku njema ya kuhitimu mwanangu. Tunakusherehekea.” Maribe aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Hata hivyo, wawili hao hawako pamoja kwa sasa.

Juliani na Brenda Wairimu

Mwanamuziki Julius Owino almaarufu kama Juliani  pamoja na mwigizaji maarufu Brenda Wairimu wako na binti kwa jina Amor Owino.

Wawili hao walikuwa wapenzi kwa muda ila ndoa yao haikufanikiwa kwa sababu zisizoelezwa.

Hata hivyo,Wairimu na Juliani wameendelea kushirikiana kwenye malezi ya mtoto wao.

Bahati na Yvette Obura

Mueni Bahati, Kevin Bahati, Gift Bahati na Diana Marua
Mueni Bahati, Kevin Bahati, Gift Bahati na Diana Marua
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki Bahati na Obura wako na binti wa miaka tano kwa jina Mueni Bahati.

Wawili hao walikuwa wapenzi ingawa walivunja uhusiano wao takriban miaka tano iliyopita.

Hata hivyo, wawili hao wameweka jambo la kuwa na mtoto pamoja wazi  huku wakifungulia binti wao ukurasa wa Instagram.

Wawili hao kwa sasa wako kwenye mahusiano mengine kila mmoja wao.

King Kaka na Chemutai Sage

Chemutai Sage na Kinga Kaka
Chemutai Sage na Kinga Kaka
Image: Hisani

Wanamuziki King Kaka na Chemutai sage wako na binti wa miaka saba kwa jina Ayanna .

Wawili hao wamekuwa wakishirikiana kwa ulezi wa binti yao licha ya kutokuwa kwenye uhusiano. 

Kwa sasa Kaka ako kwenye ndoa mtangazaji wa Switch TV, Nana Owiti.

Inadaiwa kuwa Sage alipata mimba ya King Kaka wakati moja na Bi Owiti

Prof Hammo na Jemutai

Hili ni jambo ambalo limekuja kufichuliwa hivi majuzi.

Wacheshi Hammo na Jemutai wamekiri kuwa na watoto wawili pamoja licha ya kutokuwa katika uhusiano wa wazi.

Uhusiano kati ya wawili hao umekuwa umefichwa kwa muda mrefu hadi mwezi mmoja uliopita ambapo Jemutai alilalamika faraghani kuwa Hammo hakuwa anawajibika katika ulezi wa watoto wao wawili.

Jambo hilo liliibua gumzo kubwa mitandaoni huku Hammo akiagiza kufanyika kwa vipimo vya DNA. Matokeo ya vipimo hivyo yalidhibitisha kuwa watoto hao ni wake.