WASANII WALIOGEUKA

Wasanii mashuhuri waliowahi kuhamia au kugura sekta ya injili

Siku chache zilizopita Willy Paul alieleza kuwa chuki, ubaguzi, mapendeleo na ngoma zake kukosa kuchezwa ndio sababu aligura sekta ya injili.

Muhtasari

Willy Paul, Size 8, Wahu, DNA na Amani na miongoni mwao

Wahu, Amani, Willy Paul, Size 8
Wahu, Amani, Willy Paul, Size 8
Image: Hisani

Size 8

Linet Munyali almaarufu kama Size 8 alianza kama msanii wa nyimbo za kidunia kabla ya kuhamia sekta ya injili miaka nane iliyopita.

Msanii huyo ambaye ni mke wa mcheza santuri Samuel Muraya almaarufu kama DJ Mo alitoa wimbo wake wa injili wa kwanza kwa jina ‘mateke’ mwaka wa 2013 kuashiria kuwa alikuwa ameokoka na kwa hivyo kumpiga shetani mateke.

DNA

DNA
DNA
Image: Hisani

Mwanamuziki huyo anayetambulikana kwa kibao chake ‘Banjuka’ amekuwa na taaluma ya usanii yenye utata sana.

Mwaka wa 2009, DNA alipokelewa na Kambua na Isaac Kahura  kwenye sekta ya injili na akaachilia kibao ‘Mtoto wa Sonko’ kilichoashiria kuwa yeye ni mtoto wa Mungu.

Hata hivyo, mwaka wa 2012  alieleza kuwa hali haikuwa rahisi kwenye sekta hiyo huku akitangaza kuwa amegura injili.

Aliendelea kutoa kibao cha kutumbuiza kwa jina ‘Maswali ya polisi’

Amani

Cecelia Wairimu almaarufu kama Amani ni baadhi ya wasanii wanawake walioipa jina kubwa sekta ya muziki nchini.

Alianza taaluma yake ya muziki mwaka wa 2001 ambapo aliachilia vibao ‘Tahidi’ na ‘Papii’.

Alitambulika sana kutokana na ngoma zake ‘Missing my baby’, ‘Ninanoki’ akishirikisha Nameless na ‘Usiwe mbali’

Amani aliwahi shirikishwa kwenye wimbo ‘Hands across the world’ wa msanii mashuhuri duniani R Kelly kwa jina .

Hata hivyo, mwaka wa 2018 alitangaza kuwa alikuwa ameokoka na kuingia kwenye sekta ya injili. Aliendelea kutoa nyimbo ‘My God’ na ‘Upendo’

Wahu

Nameless na Wahu
Nameless na Wahu
Image: Hisani

Wahu Kagwi ambaye ni mke wa mwanamuziki mashuhuri Nameless alianza taaluma yake ya usanii mwaka wa 2000 akiimba nyimbo za kidunia.

Nyimbo zake za kwanza ni pamoja na ‘Niangalie’, ‘Esha’ na ‘Liar’.

Kati ya nyimbo zilizompatia umaarufu mkubwa ni ‘Sweet love’ na ‘Sitishiki’.

Mwaka wa 2017, Wahu alitangaza kuwa alikuwa ameokoka na akaendelea kutoa wimbo wake wa injili wa kwanza ‘Sifa’. Baadae aliachilia ‘My Everything’, ‘Nifanane nawe’ na ‘Power Power’ akishirikisha Wahu.

Hata hivyo, utata umeibuka baada ya msanii huyo kutoa wimbo wa kimapenzi ‘This Love’ akishirikisha bwana yake, Nameless.

Willy Paul

Bila shaka mwanamuziki Willy Paul ndiye msanii wa sasa aliyekuwa na taaluma ya muziki yenye utata mwingi zaidi nchini Kenya.

Paul alianza kama msanii wa nyimbo za injili mwaka wa 2010 alipoachili kibao chake cha kwanza ‘Rabuka’.

Baadae alishirikisha  mwanamuziki tajika Gloria Muliro kwenye nyimbo ‘Sitolia’ na ‘Najitia kitanzi’ ambazo zilimpatia umaarufu mkuwa sana.

Alifanikiwa sana kwenye sekta ya injili huku akishinda tuzo la Groove mwaka wa 2012 na 2013.

Hata hivyo, msanii huyo alishangza wengi baada yake kuanza kutengeneza nyimbo za kimapenzi na kisha nyimbo za kidunia.

Alikiri kuwa alikuwa amegura injili na kuhamia sekta ya muziki wa kidunia.

Siku chache zilizopita Willy Paul alieleza kuwa chuki, ubaguzi, mapendeleo na ngoma zake kukosa kuchezwa ndio sababu aligura sekta ya injili.