'Haya huwa naona kwa movie tu!'Mengi yafichuka yaliyotendeka katika mazishi ya Ayimba

Muhtasari
  • Mengi yafichuka yaliyotendeka katika mazishi ya Ayimba
  • Sandra alidai kwamba ni shahidi kwamba dada yake Ayimba amekuwa akimchukuia muigizaji Moraa
Benjamin Ayimba akichezea timu ya taifa
Benjamin Ayimba akichezea timu ya taifa
Image: Hisani

Kocha wa Rugby marehemu, Benjamin Ayimba alizikwa nyumbani kwake kaunti yaa Siaya siku ya ijumaa huku drama ikishuhudiwa.

Bali na wanawe kuzuiliwa kuhudhuria mazishi yake, imedaiwa kwamba dada yake alisema kwamba muigizaji Moraa mama wa watoto wake ndiye alisababisha kifo chake.

KUlingana na muigizaji Sandra Dacha mambo hayo huwa anayaona kwenye filamu za Nigeria lakini aliyashuhudia na macho yake mwenyewe.

"Irene aliwaambia Maafisa kuwa Moraa ndiye aliyehusika na ugonjwa na kifo cha Baba Otienoeno na kwamba hatupaswi kuruhusiwa kuingia ndani🤦

Kwa hivyo wakati Fabs (mama ya mtoto wake mwingine ) alipompeleka Benja kortini, ilikuwa sawa?

Wakati mkewe (Caro) alimwacha kwa mtu mwingine na alirudi tu baada ya kifo chake, ni sawa sana? Mbona hii ya Moraa ndio inaleta shida?,"

Sandra alidai kwamba ni shahidi kwamba dada yake Ayimba amekuwa akimchukuia muigizaji Moraa kutoka enzi za kitambo.

"Irene umekuwa ukimchukia Moraa tangu 2012 na mimi ni shahidi. ..kila muigizaji anafahamu hii kwasababu tumekuwa tukibadilishana katika hizo group zetu za watsap

Halafu unashinda ukiita watoto wa mwanamke mwenzako chokora / bastards na wewe pia umezaa😱 Kwa hivyo ikiwa waliamua kunifukuza kutoka nyumbani, nianguke, Nani angeniokota? Je! Unataka kuchimba mchimbaji?" Aliandika Sandra.

Kupitia kwenye ujumbe mwingine Sandra alifiichua kuwa;

"Kile nimeshuhudia leo Mimi huona Tu Kwa Nigerian movies😂🤣🤣🤣 kumbe haya mambo yanafanyika kwa maisha ya kweli🤦 Aibu gani hii,"

Je tusema kwa kimombo ni 'sister-in-law from hell au vipi? ana utu wa ubinadamu?