'Mungu hafanikishi uovu,'Ujumbe wake Anerlisa kwa mashabiki

Muhtasari
  • Anerlisa Muigai awashauri mashabiki jinsi ya kuishi maisha yenye amani
  • Yaani wanamtania Mungu wao, bila ya kujali makubwa ambayo amewatendea

Mkurugenzi mkuu katika kampuni ya nero Anerlisa Muigai siku ya Jumapili alitoa ushauri wa bure kwa mashabiki wake jinsi ya kuishi kwa matakwa ya mwenyezi Mungu.

Anerlisa ambaye waliachana na mumewe msanii Ben Pol miezi chache iliyopita anaonekana kuendelea vyema na maisha yake.

Kuna baadhi ya watu ambao wamezoea kumkosea Mungu na licha yao kufahamu kuwa hiyo ni dhambi wanaitenda na kisha kuomba msamaha.

Yaani wanamtania Mungu wao, bila ya kujali makubwa ambayo amewatendea.

"Mungu hafanikishi uovu, mara tu utakapoelewa jambo hili, utakuwa na maisha ya amani sana na huwezi kuwa na ajenda mbaya sana mtu yeyote au kitu chochote," Aliandika Anerlisa.

Kwa muda sasa Anerlisa amekuwa akiwashauri mashabiki wake kufuata njia ambayo inastahili na kuacha mabaya yote.