OMONDI VS MUTUA

Ezekiel Mutua hajui kusaidia wasanii- Eric Omondi

Omondi amemsuta Mutua kwa kusitisha udhamini kwa Bahati huku akisema kuwa hakufanya lolote mbaya ila alitumia ubunifu ile aweze kugharamia majukumu yake.

Muhtasari

•Mutua kupitia bodi ya KFCB alisitisha udhamini huo kwa madai kuwa Bahati alikuwa ametoa video chafu na inayokiuka sera za ushirikiano.

Ezekiel Mutua na Erick Omondi
Ezekiel Mutua na Erick Omondi
Image: Hisani

Mcheshi tajika Eric Omondi amemsuta mkurugenzi mtendaji wa bodi ya uainishaji wa filamu nchini (KFCB), Ezekiel Mutua kwa kile amesema ni “kutounga mkono usanii”

Omondi ametoa hisia hizi kwenye mtandao wa Instagram kufuatia tukio la hivi punde ambapo Bw. Mutua alikatiza udhamini wa zaidi ya laki mbili kwa mwanamuziki Bahati.

Mutua kupitia bodi ya KFCB alisitisha udhamini huo kwa madai kuwa Bahati alikuwa ametoa video chafu na inayokiuka sera za ushirikiano.

Wakati alinipigia(Bahati) kuniomba nambari ya yule CEO(Mutua), simnajua yule jamaa wa vipindi, nilimwambia wachana na huyo hasaidiangi watu lakini hakuskia” Omondi aliandika.

Omondi alimtetea Bahati kwa kusema hakufanya lolote mbaya ila alikuwa mbunifu ili aweze kugharamia majukumu yake.

“Sidhani Bahati alifanya chochote kibaya. Sisi kama wabunifu tunahitajika kufanya hilo.. kuwa mbunifu. Bahati alifanya kile alihitajika kufanya ili kusukuma albamu yake na hivyo ndivyo unaweka chakula kwa meza. Yeye ni baba ya watoto wane bwana” Omondi alisema

Omondi alimshauri Bahati kuwa wakati mwingine anapohitaji usaidizi asiende kwa  Ma CEO(akiashiria Mutua) ila aende kwake yeye.

Siku ya Jumapili, Omondi alimpatia Bahati Sh200000 kama fidia kufuatia kusitishwa kwa udhamini wa KFCB.

Erico amewahi kuzozana na bosi wa KFCB angalau mara mbili kuhusiana na video na picha alizopakia mitandaoni.

Tarehe kumi na mbili mwezi mechi, Omondi alikamatwa na maafisa wa DCI siku moja baada ya kutangaza mkondo wa pili wa kipindi hicho. Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya uainishaji wa Filamu nchini Kenya(KFCB), Ezekiel Mutua alidai kuwa Omondi alikuwa amekamatwa kwa kukiuka masharti ya filamu na michezo ya jukwaani kwa kutengeza na kusambaza filamu za 'Wife Material'.

Mutua alisema kuwa Omondi alikuwa katengeneza na kusambaza filamu zisizoidhinishwa. Tangulia kukamatwa kwake, video iliyoonyesha wanadada wakipigana kwenye klabu alipokuwa mcheshi huyo ilikuwa inasambazwa mitandaoni. Tukio ambalo lilidaiwa kusababishwa kukamatwa kwake.

Omondi wameonekana kuzozana mara kwa mara na Mutua kutokana na kipindi hicho huku akiziita studio za Omondi madanguro mwaka uliopita.Mutua alisema kipindi hicho kuwa hatari kwa watoto na kuagiza wasanii kutengeza vipindi zilizo sawa kwa kila mtu.