'Itabidi wazoee,'Bahati awashambulia wanaotafutia albamu yake makosa

Muhtasari
  • Bahati awashambulia wanaotafutia albamu yake makosa
  • kibao cha pete yangu ambacho amemshirikisha msanii Nadia Mukami  kimevuma kwenye youtube
Bahati kwenye wimbo "Fikra za Bahati'
Bahati kwenye wimbo "Fikra za Bahati'
Image: Instagram

Msanii Bahati amekuwa akivuma kwa muda mitandaoni baada ya kutangaza kuchukua mapumziko kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

Baada yake kurejea alizidi kuvuma baada ya kufichua kwamba anaenda kutoa albamu, ambayo alizindua jumapili JUni 13.

Kati ya nyimbo ambazo ziko katika albmu yake ni kama vile, Fikra za Bahati, Pete Yngu miongoni mwa nymbo zingine.

kibao cha pete yangu ambacho amemshirikisha msanii Nadia Mukami  kimevuma kwenye youtube.

Kupitia wenye ukurasa wake Bahati alidai kwamba kuna watu ambao wamashaanza kutafuta makosa kutoka kwa albamu yake.

Msanii huyo alisema ni kawaida kwa msanii kama yeye ambaye anavuma sana mitandaoni kuonewa wivu na watu bila sababu.

Pia aliwaonya na kusema kwamba watazoea kumuona nambari moja wapende wasipende.

"Ni kawaida ukiwa unavuma nambari moja kila nambari ambaye ako wa mwisho kukuonea wivu,kwa maana hawaelewi kwanini Mungu alikuchagua na sio wao

Naskia kuna watu washaanza kutafutia albamu yangu #love like this makosa juu hawaelewi vile natrend namba 1,2 na 3

Japo kuwa itabidi wazoee kwani saa hii naongea na youtube waone vile wanaeza badilisha kanuni ndio nivume kutoka nambari moja hadi kumi

Mashabiki wangu waambieni waanze kuzoea kumuona Bahati namba moja kwani ni matendo ya Mungu," Aliandika Bahati.