JE, MUMEWE NYOTA NDOGO ASHAMRUDIA?

“Wanakuita babu lakini hujazaa na nyanya zao” Nyota Ndogo akashifu wanaosema mumewe ni mzee

Mwanamuziki huyo ameandika ujumbe maalum wa kusifia utanashati wa mumewe na kueleza hisia zake

Muhtasari

•“Yenyewe niko na bwana msupu sana. Nimekupeza kishenzi. Wanakuita babu lakini hujazaa na nyanya za. Nakupenda mpaka mbasi.” Nyota Ndogo aliandika

•Mwezi uliopita, mwanamuziki huyo kutoka Pwani alimuandika mumewe msururu wa jumbe za mapenzi kwenye mtandao wa Instagram akimsihi kumrudia. 

Nyota Ndogo na mumewe
Nyota Ndogo na mumewe
Image: Instagram

Baada ya kunyamaza kwa muda kuhusiana na uhusiano wake na mumewe, mwanamuziki Nyota ndogo kwa mara nyingine amemuandikia mpenzi wake mzungu ujumbe wa kusisimua.

Kupitia mtandao wa Instagram, Nyota Ndogo amesifia utanashati wa mumewe huku akisuta wanaosema kuwa ni mzee.

Yenyewe niko na bwana msupu sana. Nimekupeza kishenzi. Wanakuita babu lakini hujazaa na nyanya za. Nakupenda mpaka mbasi.” Nyota Ndogo aliandika

Mwezi uliopita, mwanamuziki huyo kutoka Pwani alimuandika mumewe msururu wa jumbe za mapenzi kwenye mtandao wa Instagram akimsihi kumrudia. Nyota Ndogo alidai kuwa mumewe ambaye ni mzungu kutoka Udenmarki alikuwa amemuacha na kufunga njia zote za mawasiliano baada yake kumtania kuwa na mimba siku ya "Fools Day'

Hatimaye mumewe alijibu jumbe zake kupitia WhatsApp akimwambia kuwa anampeza. 
"Jamani amkeni leo nakesha nimeblue tikiwa na nikaitwa bibi. Amenipeza jamani amkeni. Nimeshindwa la kujibu. Naanzaje kujibu jamani silali leo ntaangalia tu huu ujumbe" Msanii huyo aliandika wiki mbili zilizopita baada ya kupokea ujumbe wa mumewe.

Kufuatia ujumbe ambao alimuandikia mumewe asubuhi ya Almisi ni ishara kuwa huenda wawili hao wamerudiana na wako kwenye  mawasiliaIiano mema.