"Hamuoni haya?" Akothee akosoa wanaume ambao hawawajibiki kulea watoto wao

Alisema kuwa ili mwanaume kuhitimu kuitwa baba anahitajika kuwajibika katika ulezi wa mwanawe.

Muhtasari

•"Je, huoni haya kuona wanaume wengine wakipeleka watoto wao shuleni?  Huonin haya kuona baba wengine wakipeleka watoto wao kununua bidhaa? Hujihisi mwenye hatia ukiona kina baba wengine wakipeleka watoto wao likizo? Hauoni haya?" Akothee aliuliza.

•Kwenye maadhimisho ya siku ya kina baba duniani, aliwasherehekea wote watatu huku akiandikia kila mmoja wao ujumbe maalum kwenye mtandao wa Instagram.

Akothee
Akothee
Image: Instagram

"Wafadhili wa mbegu za kiume" ndivyo mwanamuziki na mwanabiashara maarufu Akothee amewaita wanaume ambao kazi yao ni kupatia wanawake mimba kisha wanakosa kuwajibika kwenye malezi.

Dunia ilipokuwa inaadhimisha siku ya kina baba  Jumapili, Akothee alitumia fursa hiyo kuwakosoa wanaume ambao wametelekeza majukumu yao katika ulezi kupitia mtandao wa Instagram.

"Mtoto ana mama  mzazi mmoja na baba mzazi  mmoja" ndio ulikuwa ujumbe wa Akothee.

Alisema kuwa ili mwanaume kuhitimu kuitwa baba anahitajika kuwajibika katika ulezi wa mwanawe.

"Wanaume kumbukeni kuwa kupata mtoto na mwanamke peke yake haifanyi uhitimu  kuitwa baba. Inahitaji uwajibikaji kamili na kuchangia kabisa maishani mwa watoto wako." Akothee aliandika.

"Wewe ndiye baba mzazi ndio, lakini kando na kufurahia tendo la ndoa na mama ya mtoto huyo, mchango upi umetoa  katika maisha ya watoto wako." Aliendelea kuwakosoa wanaume wasiowajibika.

Mwanzilishi huyo wa Akothee Safaris miongoni mwa kampuni zingine aliwauliza kana kwamba wanaona hayakuona wanaume wengine wakiwajibika ilhali wao wamekosekana kabisa katika maisha ya watoto wao.

"Je, huoni haya kuona wanaume wengine wakipeleka watoto wao shuleni?  Huonin haya kuona baba wengine wakipeleka watoto wao kununua bidhaa? Hujihisi mwenye hatia ukiona kina baba wengine wakipeleka watoto wao likizo? Hauoni haya?" Akothee aliuliza.

Aliwasherehekea wanawake ambao wanalea watoto wao wakiwa peke yao bila usaidizi wa baba wa mtoto huku akisema kuwa walikuwa wamekubali kuchukua majukumu ya baba na mama. Hata hivyo, aliwapongeza kina baba wanaowajibika na kuwatakia siku njema ya kina baba.

Mwanamuziki huyo ako na watoto watano ambao amepata na wanaume watatu tofauti; Mkenya mmoja, Mfaransa na raia wa Uswidi mmoja.

Mabinti wake watatu ndio watoto wa kwanza ambao alipata na  aliyekuwa mume wake wa kwanza, Jared Okello. 

Baada ya hapo alipata mvulana mmoja na mzungu kutoka Uswidi na kitinda mimba wake alipata na mzungu mwingine kutoka Ufaransa.

Kwenye maadhimisho ya siku ya kina baba duniani, aliwasherehekea wote watatu huku akiandikia kila mmoja wao ujumbe maalum kwenye mtandao wa Instagram.