Hongera: Shiksha Arora arejea kwenye runinga baada ya mwaka mmoja

atakuwa anatangaza kwenye runinga ya KBC

Muhtasari

•"Mwaka mmoja baadae, nimerejea, nimerejea kama kwamba sikuwa nimeondoka. Ungana nami katika stesheni ya KBC ambako ni maskani yangu mapya.  Shukran kwa kusimama nami, ungana nami kila Ijumaa saa tatu. Ni wakati wa kutengeneza miujiza na KBC" Arora aliandika.

Shiksha Arora
Shiksha Arora
Image: Instagram

Baada ya kupoteza kazi yake ya kusoma habari katika stesheni ya runinga ya K24 kufuatia kupunguzwa kwa wafanyakazi mwaka jana, mtangazaji maarufu Shiksha Arora amerejea tena kwenye runinga.

Arora, ambaye kwa muda amekuwa akifanya kazi katika stesheni ya radio ya East FM sasa atakuwa anatangaza kwenye runinga ya KBC TV kuanzia Ijumaa ijayo.

Mtangazaji huyo ambaye ana ufuasi mkubwa mitandaoni alitangaza kurejea kwake asubuhi ya Jumatatu.

"Mwaka mmoja baadae, nimerejea, nimerejea kama kwamba sikuwa nimeondoka. Ungana nami katika stesheni ya KBC ambako ni maskani yangu mapya.  Shukran kwa kusimama nami, ungana nami kila Ijumaa saa tatu. Ni wakati wa kutengeneza miujiza na KBC" Arora aliandika.

Wanamitandao wengi wameendelea kumpongeza mwanadada huyo ambaye anasifika sana kwa urembo wake na urafiki mkubwa anaowaonyesha mashabiki wake.

Wengine ambao wamerejea kwenye stesheni hiyo ni pamoja na Fred Indimuli ambaye alipoteza kazi yake pamoja na Arora, Harith Salim, Tom Mboya, Juma Ballo na Cynthia Nyamai.

Mhariri mkuu wa KBC ameeleza kuwa mabadiliko hayo ya,eletwa na mabadiliko kwenye soko na mahitaji ya watazamaji.