"Napenda watoto sana" Vera akanusha madai kuwa aliwahi avya ujauzito

Vera ambaye ana ujauzito wa miezi tano amesema kuwa hii ni mara yake ya kwanza kuwa mjamzito na hajawahi kuwa katika hali ile tena

Muhtasari

•"Nimeskia fununu kuwa kuna mmoja wapenzi wangu wa  hapo awali ambaye alidai niliavya mimba yake. Hayo si kweli. Nawapenda watoto sana. Siwezi kuwa mjamzito kisha niavye mimba ile" Alisema Vera

•Ommy Johnson ambaye ni raia wa Nigeria alisema kuwa Vera hakuwa mwaminifu na alitoa ujauzito wake ndio maana wakatengana.

Vera Sidika
Vera Sidika
Image: Instagram

Mwanasoshalaiti Vera Sidika amekanusha madai kuwa aliwahi avya ujauzito wa mmoja wa wanaume ambao amewahi kuchumbia.

Vera ambaye ana ujauzito wa miezi tano amesema kuwa hii ni mara yake ya kwanza kuwa mjamzito na hajawahi kuwa katika hali ile tena.

Akijibu shabiki mmoja katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram, Vera amekanusha fununu kuwa aliwahi avya mimba ya mpenzi wake wa hapo awali.

"Nimeskia fununu kuwa kuna mmoja  wa wapenzi wangu wa  hapo awali ambaye alidai niliavya mimba yake. Hayo si kweli. Nawapenda watoto sana. Siwezi kuwa mjamzito kisha niavye mimba ile" Alisema Vera

Vera amesema kuwa huwa anachukua tahadhari kubwa anaposhiriki tendo la ndoa ili kuzuia kupata mimba.

"Wakati sina mchumba huwa natahadhariu. Nikiwa kwenye Uhusiano, huwa natumia dawa za kuzuia ujauzito kila wakati ili kuzuia ujauzito kwani sikuwa tayari" Vera alisema

Vera ambaye anachumbia mwanamuziki Brown Mauzo kwa sasa amesema kuwa anatumai kupata watoto watatu. Amesema kuwa atafichua jinsia ya mtoto aliyebeba mnamo Julai 3.

Hapo awali, mmoja wa waliowahi chumbia mwanasoshalaiti huyo alitangaza wazi kuwa sababu moja iliyomfanya kutengana naye ni kuwa aliavya.

Ommy Johnson ambaye ni raia wa Nigeria alisema kuwa Vera hakuwa mwaminifu na alitoa ujauzito wake ndio maana wakatengana. Wawili hao walitengana mwaka wa 2017 baada ya kuchumbiana kwa kipindi kifupi. 

Vera hata hivyo alikanusha madai hayo na kusema kuwa Johnson alikuwa mkatili na alikuwa akimdhulumu.

Sio hayo tu, mwaka wa 2018 fununu zilienea sana mitandaoni kuwa Vera aliavya ujauzito wa Otile Brown ambaye walikuwa wakichumbiana naye. 

Hata hivyo, mwanasoshalaiti huyo alikanusha hayo pia na kueleza kuwa alikuwa akitumia dawa za kuzuia ujauzito kwa wakati wote.