'Sijawahi mchukia Huddah Monroe,'Mwanasosholaiti Vera Sidika asema

Muhtasari
  • Vera Sidika aweka wazi kwamba hajawahi mchukia Huddah

Kwa muda sasa mwanasosholaiti Vera Sidika amekuwa akivuma baada ya kufichua ujauzito wake.

Vera ambaye anachumbia mwanamuziki Brown Mauzo kwa sasa amesema kuwa anatumai kupata watoto watatu.

Amesema kuwa atafichua jinsia ya mtoto aliyebeba mnamo Julai 3.

Akijibu shabiki mmoja katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram, Vera amekanusha fununu kuwa aliwahi avya mimba ya mpenzi wake wa hapo awali.

Pia katika kipindi hicho, mmoja wa mashabiki wake alimuuliza kama amewahi mchukia mwanasosholaiti mwenzake Huddah Monroe ambapo alikanusha madai hayo.

Pia alifichua kwamba Huddah alikuwa rafiki yake mwaka wa 2009 alipokuja nchini kenya kwa mara ya kwanza.

"Sijawahi, hata mara moja kumchukia Huddah, awali tulikuwa marafiki nilipokuwa mgeni jijini Nairobi mwaka wa 2009-2010," Alisema Vera.

Mnamo mwaka wa 2019 uvumi ulienea kuwa wawili hao wana ugomvi, huku vita vya maneno kati ya wawili hao vikishuhudiwa na mashabiki mitandaoni.