'Nilitaka kuwa rubani,'Diana Marua asema

Muhtasari
  • Diana Marua ni miongoni mwa wake wa wasanii na anafahamika sana kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
  • Kwa sasa yeye na mumewe Bahati wako Tanzania kuhudhuria hafla ya Rayvanny
Diana Marua
Image: Hisani

Diana Marua ni miongoni mwa wake wa wasanii na anafahamika sana kupitia kwenye mitandao ya kijamii hasa youtube.

Kwa sasa yeye na mumewe wako nchini Tanzania kuhudhuria hafla ya mwanamuziki Rayvanny.

Wanamitandao wanatarajia 'kolabo ya power' baina ya Bahati Rayvanny.  Diana anaonekana kufurahia ziara yake alipiga picha na rubani wa ndege walimoabiri ili kuweka kama kumbukumbu.

Baada ya kupakia picha hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram, alisema kwamba daima alitaka kuwa rubani maishani mwake.

Hata hivyo hakueleza kilichomzuia kuafikia ndoto yake ya kuwa rubani kama alivyotarajia maishani, huku baadhi ya mashabiki wakisema kwamba alikula karo ya shule.

"Mnajua nini nilikuwa niwe rubani katika maisha yangu,tulisafiri salama hadi Dar Es Salaam," Aliandika Diana.

Hizi hapa baadhi ya semi za wanamitandao;

meivin_kelvin: Pilot Diana😂😂❤️❤️Will miss you my mentor an it’s good to hear you got there safe and sound🙏🙏🙏💯💯❤️

jaydenadypinchez: Ulikula fees

mikesledd_dilar: Looking good ❤️❤️❤️

Pia alimpongeza Rayvanny kwa kazi yake nzuri ambayo anaendelea kufanya.