ILIKUWA VIPI?

Hamo ataja sababu za kutoka Royal Media

Alisema kuwa hakukosana na yeyote

Muhtasari

•Mcheshi Herman Kago almaarufu kama Prof Hamu amekanusha madai kuwa alifutwa kazi ya utangazaji katika kituo cha redio alichokuwa anafanyia kazi.

•Mcheshi huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa kupitia kipindi cha Churchill Show alisema kuwa kufanya kazi kwenye runinga kulimfunza kuwa hustler, jambo ambalo hangeweza kufanya wakati alikuwa anafanya kazi kwa redio.

Profesa Hamo
Profesa Hamo
Image: Instagram

Mcheshi Herman Kago almaarufu kama Prof Hamu amekanusha madai kuwa alifutwa kazi ya utangazaji katika kampuni ya Royal Media.

Amefutilia mbali madai hayo na kusema kuwa hizo ni fununu ambazo hazina msingi.

Katika mahojiano na Jalango katika kipindi cha Bonga na Jalas siku ya Jumanne, Hamo alieleza kuwa aliondoka kwa hiari yake mwenyewe.

Alipoulizwa kwa nini aliacha kazi wakati uchumi unaangamizwa na janga la Korona, Hamo alisema kuwa roho yake ilimshawishi kufuata mambo anayoamini.

"Niliamua kuwa kwa maana nilikuwa nimejiunga na redio ili kusoma, hakuna vile ningekaa pale milele. Hauwezi kaa shule milele. Mimi ni kijana, nahitaji kuenda nje na kuhustle(Kufanya kazi mbalimbali). Niligundua pale kwa redio singeweza kuhustle, ati nitoke hapo niende nizurure? Usingizi peke yake ulikuwa unakukubali??" Hamo alieleza Jalas.

Mcheshi huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa kupitia kipindi cha Churchill Show alisema kuwa kufanya kazi kwenye runinga kulimfunza kuwa hustler, jambo ambalo hangeweza kufanya wakati alikuwa anafanya kazi kwa redio.

"Baada ya kufanya kazi kwa redio kwa kipindi cha mwaka mmoja niligundua singeweza kukaa hivo, ati hii mshahara nikae nayo. Kama una nia kubwa ya kuwa tajiri, hauweza pata utajiri ukiwa umeajiriwa.`Haijalishi mapato ambayo unapata, unataka zaidi" Hamo aliendelea kusema.

"Niligundua kuwa mimi ni mwuzaji, na sisongi mbele kwa kuwa mimi si mtu wa kawaida. Watu wa kawaida hukaa wameajiriwa mahali pamoja hadi wapate kazi nyingine, wachache sana hufanya hivyo na mimi si mmoja wao. Napenda kufuata roho yangu, kitu nataka kufanya naenda huko nje na nafanya" Alisema.

Alisema kuwa hakuna mtu yeyote ambaye walikosana naye. Alisema kuwa alizungumza na mmoja wa wakubwa wake kuhusiana na ambo hilo.

Mcheshi huyo pia alifichua kuwa alizungumza na Jemutai kuhusiana na uhusiano wao na  wakakubali kusuluhisha mzozo.

Wawili hao wametangaza  kuwa iku ya Ijumaa watakuwa na kipindi ambapo watakuwa wanazungumzia yaliyojiri wakati habari za uhusiano wao zilienea kote nchini.