Siko tayari kuendeleza 'beef' na mtu-Alikiba asema

Muhtasari
  • Alikiba aweka wazi hana chuki na mtu yeyote
  • Kwa muda sasa Alikiba na Diamond walidaiwa kuwa na chuki, jambo ambalo wasanii hao wawili walitupilia mbali
ali-kiba
ali-kiba

Msanii wa bongo flava kutoka Tanzania Alikiba akiwa kwenye mahojiano aliweka wazi kwamba hayuko tayari kuendeleza chuki na mtu yeyote.

"Siko tayrai kuendeleza brrf na mtu yeyote, kama hiyo 'Beef' sio ya biashara, kwa mfano kuanzisha chuki na mtu huwa inaharibu mambo mengi kama uhusiano," Alisema Alikiba.

Kwa muda sasa Alikiba na Diamond walidaiwa kuwa na chuki, jambo ambalo wasanii hao wawili walitupilia mbali.

"Huwa sifuatilii chuki, na siwezi bishana na wasanii wenzangu kwa maana hainisaidii kuunda muziki wangu

Huwa nasaidia kila mtu awe ananisaidia pia au la, kile nataka ni kuwa na ukaribu na mashabiki wangu na kuunda muziki mzuri,"

Alikiba aliweka wazi kwamba anaenda kutoa albamu yake mwaka huu na mashabiki wanapaswa kuwa tayari kwani itakuwa ya kushangaza.

Huku akizungumzia uhusiano wake na gavana wa Mombasa Joho, alisema kwamba amekuwa mtu wa karibu kwake na familia yake.

"Nimejifunza vitu vingi kutoka kwa Joho kutokana na uzalendo wake sio tu kwa watu wa Mombasa ila kwa Wakenya wote

"Yeye ni kama ndugu kwangu, ni rafiki yangu mzuri sana," Alisema Alikiba.