(+Video) Lava Lava alia studioni baada ya aliyekuwa mpenziwe, Lulu Diva kukataa ombi la msamaha

Lava Lava alionekana akiingia studioni ambako Lulu alikuwa anahojiwa huku amebeba shada la maua na kupiga goti mbele ya Lulu.

Muhtasari

β€’Mpango wake wa kujaribu kumshangaza Lulu na kumuomba msamaha alipokuwa kwenye mahojiano katika kituo cha redio cha Wasafi haukuenda kama alivyotarajia.

Lava Lava
Lava Lava
Image: Instagram

Juhudi za mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za bongo, Abdul Juma almaarufu kama Lavalava kumuomba msamaha aliyekuwa mpenzi wake Lulu Diva zimeendelea kugonga mwamba.

Mpango wake wa kujaribu kumshangaza Lulu na kumuomba msamaha alipokuwa kwenye mahojiano katika kituo cha redio cha Wasafi haukuenda kama alivyotarajia.

Kwenye video moja ambayo ilirekodiwa katika studio za Wasafi FM siku ya Ijumaa, Lava Lava anaonekana akilia baada ya ombi lake la msamaha kukataliwa.

Lava Lava alionekana akiingia studioni ambako Lulu alikuwa anahojiwa huku amebeba shada la maua na kupiga goti mbele ya  Lulu.

Mwanamuziki huyo wa kikundi cha WCB alipojaribu kumgusa Lulu,  kwa dharau alionekana kuangalia pande nyingine na kumuagiza amuache.

"Abdul niache, sitaki!  Ningelijua singekuja hapa, naomba niache!" Lulu alisema kabla ya kuamka kuelekea kwenye ukuta.

Lulu ambaye alionekana kughadhabishwa na kitendo hicho alionekana kuchukua maua aliyokuwa amebeba Lava Lava na kuyatupa chini. Baada ya hapo alitoka nje kwa hasira.

Lava lava alijaribu kumfuata ila baada ya hatua kidogo anarudi ndani huku akionekana mwenye kuvunjika moyo.

Wengine waliokuwa pale studioni walijaribu kumfariji Lava lava aliyekuwa amejawa na maumivu moyoni.

WATCH WASAFI TVπŸ“Ί AZAM - 411 | DSTV - 296 | ZUKU - 028 | STAR TIMES - 444 & 333 | COCONUT TV - 20 | DODOMA CABLE - 113 LISTEN WASAFI FM πŸ“» 88.9 DAR/ZNZ/PWANI πŸ“» | 104.1 DODOMA πŸ“» | 94.5 ARUSHA πŸ“» | 97.3 MBEYA πŸ“» | 94.9 MWANZA πŸ“» | SHINYANGA 106.3 πŸ“» | KIGOMA 101.7 πŸ“» Follow Us On: INSTAGRAM: http://instagram.com/wasafitv || http://instagram.com/wasafifm/ TWITTER: https://twitter.com/wasafitv || https://twitter.com/wasafifm/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/wasafitv/ π‘ͺπ’π’‘π’šπ’“π’Šπ’ˆπ’‰π’• Β©2021 π‘Ύπ’‚π’”π’‚π’‡π’Š π‘΄π’†π’…π’Šπ’‚. 𝑨𝒍𝒍 π’“π’Šπ’ˆπ’‰π’•π’” 𝒓𝒆𝒔𝒆𝒓𝒗𝒆𝒅. #wasafi #wasafitv #wasafifm

Mapema wiki iliyopita Lava Lava alimuandikia Lulu ujumbe wa kuomba msamaha kwenye ukurasa wake wa Instagram  akisimulia maumivu aliyokuwa akipitia.

"Dah Usiku Wajana Ndosijalala Kabisa Lulu Kiukweli Achatu Ifike Mahali Mtu Aweke Wazi Penzi Kikohozi Alijifichi Nakupenda Lulu Bora Niwe Mtumwa Kwako Hakuna Jinsi inaenda Wiki Sasa Hatuelewani Naumia Binadamu Tumeumbiwa Kukosea Hakuna mkamilifu Samahani Sana Narudia Tena Samahani nisamehe Mwenzako Plz " Aliandika Lava Lava.