Hongera! Willis Raburu asherehekea baraka ya mtoto miezi 18 baada ya kupoteza binti

Mtangazaji Willis Raburu na mpenzi wake Ivy Namu wamemkaribisha duniani mwanao wa kwanza.

Muhtasari

β€’Siku ya Jumatatu, mtangazaji huyo wa Royal Media alifichua habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo kupitia mtandao wa Instagram.

β€’Mwaka uliopita Raburu alitengana na aliyekuwa mke wake Mary Prudence ambaye walikuwa wamefunga ndoa mwaka wa 2017.

Image: WILLIS RABURU

Mtangazaji Willis Raburu na mpenzi wake Ivy Namu wamemkaribisha duniani mwanao wa kwanza.

Mtangazaji huyo wa Royal Media alifichua habari za kuzaliwa kwa mtoto wake kupitia mtandao wa Instagram siku ya Jumatatu.

Ingawa hakupeana habari nyingi kuhusiana na hayo, Raburu ambaye alionekana kujawa na bashasha alipakia picha akiwa ameshika mkono wa mtoto na kuiambatanisha na wimbo wa kumsifu Mungu.

Image: WILLIS RABURU

Kwenye picha nyingine ambayo alipakia pale alionekana akitabasamu huku ameshika viatu vya mtoto.

Raburu amekuwa akichumbiana na mpenziwe Ivy Namu kutoka Uganda kwa muda sasa. Hata hivyo, wawili hao wamekuwa wakiweka uhusiano wao kisirisiri.

Mwaka uliopita Raburu alitengana na aliyekuwa mke wake Mary Prudence ambaye walikuwa wamefunga ndoa mwaka wa 2017.

Mwezi wa Januari mwaka uliopita, Raburu na Prudence waliomboleza binti wao ambaye alizaliwa kama ameaga tayari.

Wakenya ikiwemo wasanii na watu mashuhuri walijumuika kumpongeza Raburu kwa baraka hiyo. Hizi hapa baadhi ya jumbe za pongezi

annitahraey

Congratulations my guy πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ

honalinur

Congratulations BAZUU

ogadaolunga

Bazu πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

barakjacuzzi

Congrats bro!!!We not sleeping on them arm gains tooooπŸ”₯πŸ’ͺ🏾πŸ’ͺ🏾

bienaimesol

β€οΈπŸ™ŒπŸ”₯

patrickigunza

Answered prayers!!! You are blessed bro man. πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ‘ŠπŸΏ

Kutoka kwa Radio Jambo, Hongera Willis Raburu!!