Jamaa wa 'Nitakufinya' aeleza ghadhabu iliyofanya atishie kumfinya mwenzake

Matendechere alisema kuwa hakupendezwa na maneno ambayo yalikuwa yakizungumziwa pale kwenye mahojiano hayo.

Muhtasari

•Mwanaume aliyetambulishwa kama Charles Musyoka alikuwa akihojiwa kuhusiana na madhara ya nguvu za umeme haramu wakati mwanaume mwingine aliyekuja nyuma yake alidakiza mahojiano hayo na kumuagiza aache kuongelea mambo ya stima.

•Matendechere alieleza kuwa aliamua kuingilia kati ili kutetea kampuni ya kusambaza stima ya KPLC kwani alihisi walikuwa wanaharibiwa jina.

Nitakufinya
Nitakufinya
Image: K24

"Nitakufinya" 

"Finya"

Haya ni maneno ambayo yamekuwa midomoni mwa Wakenya na kuenea sana mitandaoni siku za hivi karibuni.

Video ambayo imedondolewa kutoka kwa ripoti iliyofanywa na stesheni ya runinga ya K24 miaka nane iliyopita imesisimua sana wanamitandao.

Mwanaume aliyetambulishwa kama Charles Musyoka alikuwa akihojiwa kuhusiana na madhara ya nguvu za umeme haramu wakati mwanaume mwingine aliyekuja nyuma yake alidakiza mahojiano hayo na kumuagiza aache kuongelea mambo ya stima.

"Asiongee mambo ya stima aongee mambo ingine. Mambo ya stima aachie watu wa stima. Mambo ya stima achia watu wa stima waongee. Wacha kuongea mambo ya stima, ongea unataka serikali ikupatie kazi" Jamaa huyo alimwambia Musyoka.ambaye ametambulishwa kama Joram Matendechere alimwambia Musyoka.

Wawili hao walionekana kujibizana  kwa kipindi kifupi huku Musyoka akimuarifu kuwa alikuwa na kazi tayari na alikuwa tu akijibu swali aliloulizwa.

Katika mahojiano ya moja kwa moja na Jalongo kwenye kipindi cha Bonga na Jalas siku ya Jumatatu, jamaa aliyemtishia Musyoka na ambaye alitambulishwa kama Aaron Matendechere alifichua ghadhabu iliyomfanya atake kumfinya mwenzake.

Matendechere alisema kuwa hakupendezwa na maneno ambayo yalikuwa yakizungumziwa pale kwenye mahojiano hayo.

Alieleza kuwa aliamua kuingilia kati ili kutetea kampuni ya kusambaza stima ya KPLC kwani alihisi walikuwa wanaharibiwa jina.

"Niliona vile kulikuwa kunaongelelewa nikaona nitetee watu wa Kenya Power. Ilikuwa kutetea watu wa Kenya Power" Matendechere alisema.

Matendechere alikanusha madai ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakidai kuwa hasira yale iliibuka  kwani pia yeye alikuwa ameingiza stima kiharamu kwenye biashara yake ya hoteli na kuonyesha filamu.

'Kwa upande wangu niko na mita na huwa nalipia, hata ujumbe niliotumiwa niko nao. Mimi sikuwa naingiza stima kiharamu kama watu wanavyosema." Matendechere alisema.

Hata hivyo, Matendechere alisema kuwa hakuwahi mfinya Musyoka licha ya kumpa tishio hilo.

Wawili hao walipatana kwa mara ya kwanza kwenye kipindi hicho cha Jalango na wakasalimiana kuashiria kuwa hawana ugomvi wowote.