(+Video) Omosh Kizangila amerejea! Wanamitandao waridhishwa na hatua ya Omosh kurejelea uigizaji

Wawili hao walitoa sinema yao ya kwanza siku ya Jumatano na imepokelewa vyema na mashabiki huku wengi wakionekana kufurahishwa na hatua hiyo

Muhtasari

•Mwigizaji huyo ambaye amekosekana sana kwenye ulingo wa sanaa ameshirikishwa na mwigizaji Steven Oduor Dede almaarufu kama DJ Shiti kwenye kipindi  cha YouTube cha 'Sinema Za Shiti.'

•Mashabiki wengi wameeleza kuridhika kwao kuona hatimaye Omosh ameamua kufanya kitu ambacho kinaweza mpatia mapato yake mwenyewe badala ya kuombaomba.

DJ SHITI NA OMOSH WAKIIGIZA
DJ SHITI NA OMOSH WAKIIGIZA

Baada ya kuibua gumzo kote nchini kutokana na mazoea ya kuomba misaada na tuhuma za uraibu wa pombe, mwigizaji wa Tahidi High Joseph Kinuthia almaarufu kama Omosh hatimaye amerejelea sanaa ya uigizaji.

Mwigizaji huyo ambaye amekosekana sana kwenye ulingo wa sanaa ameshirikishwa na mwigizaji Steven Oduor Dede almaarufu kama DJ Shiti kwenye kipindi  cha YouTube cha 'Sinema Za Shiti.'

Wawili hao walitoa sinema yao ya kwanza siku ya Jumatano na imepokelewa vyema na mashabiki huku wengi wakionekana kufurahishwa na hatua hiyo.

Mashabiki wengi wameeleza kuridhika kwao kuona hatimaye Omosh ameamua kufanya kitu ambacho kinaweza mpatia mapato yake mwenyewe badala ya kuombaomba.

Sinema hiyo imegusia baadhi ya masaibu Omosh alikuwa amekumbwa nayo.

Mwezi uliopita Omosh aliomba msaada wa Camera na vifaa vya kusaidia kurekodi video akiahidi kuwa huo ndio msaada wa mwisho atakuwa anawaomba Wakenya.

"Mimi mwenyewe naweza taka ninunuliwe tu kacamera, tripod na kalights tuwili na mic nitakuwa nimewaacha. Huyo jamaa atakuwa amenipatia capital ingine ajabu" Omosh alisema akiwa kwenye mahojiano.

Mwanamuziki kutoka Pwani, B Classic alijitolea kumtimizia maombi yake kwa kumnunulia vitu alizokuwa akitamani.

Kuna matumaini ya sinema zingine kutoka kwa Omosh kwani kulingana na maelezo ya sinema aliyoshirikishwa, hicho kilikuwa kipande cha kwanza tu.