Harmonize awashauri mashabiki kufuata njia za Yesu

Muhtasari
  • Harmonize awashauri mashabiki wake huku akiahidi kufanya collabo na mtoto wa miaka 3
68982464_381056136120833_6438164767961324750_n
68982464_381056136120833_6438164767961324750_n

Siku chachee baada ya msanii wa Bongo Harmonize kudaiwa huwa ananunua wataamaji wa youtube ili vibao vyake vivume, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amezungumza akitumia mfano wa Yesu.

Kupitia kwenye ujumbe wake alioupakia kwenye ukurasa wa instagram aliwashauri mashabiki wake wasiwaze sana kuhusu yale watu wengine wanasema kuwahusu kwani Yesu alisemwa sana na hakujiulizia.

Alizungumza haya baada ya kupakia video ya mtoto wa miaka mitatu ambaye alikiri kwamba anampenda Harmonize.

Pia mtoto huyo alidai angependa kuimba collabo na msanii huyo ambaye aliahidi kwamba ataimba na mtoto huyo.

"USISHANGAE KUONA WALIMWENGU WAKISEMA NIMEMNUNUA HUYU MTOTO WA MIKA MITATU (3) HIII IWE FUNZO KWAKO WEWE UNAESOMA HAIJALISHI WATU WANAONGEA NINI KUHUSU WEWE USIJIBU WALA USIUMIE ALISEMWA KRISTU & MTUME MUHAMMADI WEWE NI NANI ....??? SHUKURU MUNGU KWA YOTE SONGA MBELE ..!! KAMA JESHI ANAVYOFANYA 🙏🙏🙏 LET'S GET IN THE STUDIO IM READY ...!!! NAMI NAIMBA NA WEWE 🥰🥰 OYAAA UMEITAZAMA," Alisema Harmonize.