'Mimi ni tishio kwangu mwenyewe' Willy Paul adai kuwa ndiye msanii bora Afrika Mashariki

Amedai kuwa tishio lake kwenye muziki wa kidunia Afrika Mashariki ni yeye peke yake.

Muhtasari

•"Hakuna mshindani. Hakuna tishio. Mimi ni tishio kwangu mimi mwenyewe... Kanda la  Afrika Mashariki kunaye kweli, aai bado" Wily Paul alisema.

Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Mwanamuziki Willy Paul amejigamba kuwa ndiye mwanamuziki bora wa nyimbo za kidunia nchini na Afrika Mashariki.

Willy ambaye aligura sekta ya injili takriban miaka miwili iliyopita amedai kuwa hana mshindani wala tishio lolote katika kanda ya Afrika Mashariki.

Akizungumza na Mpasho, mwanamuziki huyo aliyekumbwa na utata si haba amedai kuwa tishio lake kwenye muziki wa kidunia Afrika Mashariki ni yeye peke yake.

"Hakuna mshindani. Hakuna tishio. Mimi ni tishio kwangu mimi mwenyewe... Kanda la  Afrika Mashariki kunaye kweli, aai bado" Wily Paul alisema.

Hata hivyo, mwanamuziki huyo amesema kuwa anapendezwa sana na kazi ya wanamuziki wa Nigeria kama vile Davido, Burna Boy na Wizkid na wanampa changamoto kufanya bidii ili kuwafikia.

"Afrika nawaangalia sana Burna Boy, Wiz Kid na Davido. Wameset bars, ukiwaangalia wanakupa changamoto. Naweza taka siku moja Mungu anifungulie njia kama wao ama hata bora kuwaliko" Paul alisema.

Wiki iliyopita msanii huyo alitoa wimbo 'Lenga' akimshirikisha mwanamuziki wa nyimbo za injili Size 8 ambao alizungumzia sababu zake kugura injili.